24/08/2022
UGUMBA AU KUTOSHIKA MIMBA KWA WANANDOA
(1) Nini maana ya ugumba au kushindwa kushika mimba?
-- Ugumba ni kushindwa kushika mimba baada ya miezi 12 ya kufanya tendo la ndoa pasipo kinga au miezi 6 kwa wanawake wenye zaidi ya miaka 35.
Hii maana ya ugumba imerudia kulingana na taarifa ambazo zimeonesha 50% ya ndoa hupata ujauzito ndani ya miezi mitatu, 75% - 82% ndani miezi sita, na 85 - 92% ndani ya miezi 12, lakini hutambua kadri umri uongezekapo ndipo uwezo wa kushika mimba hushuka.
JE SHIRIKA LA AFYA DUNIANI HUSEMA NINI JUU YA UGUMBA
Kulinga na WHO huutambua ugumba k**a ni moja ya kilema na uzingatifu wa huduma bora kwa tatizo hili huangukia katika haki za watu wenye ulemavu.
Karibia wanawake milioni 34, mara nyingi kutoka katika nchi zinazoendelea , ugumba hutokana na matatizo ya kuathiriwa na bakteria sehemu za uzazi ambao hupelekea kutokwa na uchafu na utoaji wa mimba pasipo usalama.
JINSI YA KUMHOJI AU KUMCHUNGUZA MGONJWA
(1) NINI UCHUNGUZI WA AWALI
-- katika ndoa zote zenye kuonesha changamoto hii ya kushindwa kushika mimba, uchunguzi wa awali huhusisha muda sahihi wa kufanya ngono na kujadili visababishi vingine k**a sigara, pombe, caffeine ambayo hupatikana kwenye soda - kahawa - majani ya chai, uzito kupitiliza, matumizi ya uzazi wa mpango, magonjwa yanayohusiana na kutokwa uchafu. Uchunguzi huu wa awali husaidia kutambua k**a changamoto hio chanzo chake ni mwanaume
NB: Uchunguzi huu utahusisha wahusika wote wa ndoa yaani mwanaume na mwanamke.
- Uchunguzi huu utahusisha uchunguzi wa shahawa za mwanaume, kuthibitisha upevukaji wa yai kwa mwanamke, uchunguzaji wa mirija ya uzazi
(2) MATATIZO YA KISAIKOLOJIA AMBAYO HUHUSIANA NA UGUMBA
-- Matatizo ya kisaikolojia huwa ni sababu ya kutoshika ujauzito. Saikolojia hii inaweza kuyumbishwa si na vipimo na matibabu ya tatizo la ugumba bali na kitendo cha kujirudia cha kuwa na matumaini alafu matumaini hayo kupotea tena kwa kila njia mpya inapojaribiwa pasipo mafanikio ya kushika ujauzito. Kutengwa na familia na marafiki husababisha kuathirika zaidi kisaikolojia
-- Matibabu ya kisaikolojia huhitajika kutolewa mapema
(3) SABABU ZILIZOPO UPANDE WA MWANAMKE
Ijapokuwa wanandoa wote wanaweza kuhusika kusababisha tatizo hili lakini mwanamke anapaswa kuchunguzwa zaidi kwasababu ndie hubeba mimba.
👉 Matatizo ya mfumo wa hedhi huwa yenye asilimia kubwa ya kusababisha kushindwa kushika ujauzito. Matatizo hayo ni k**a kasoro katika upevukaji wa yai na kasoro katika tumbo la uzazi, changamoto hizi zinaweza kupelekea mwanamke kutoingia kwenye hedhi au hedhi isioeleweka au hedhi fupi.
-- Kwa uchunguzi wa karibu wa historia ya mgonjwa na vipimo vya maabara inaweza kusaidia kujua kasoro katika (1) tezi kuu (hypothalamic au pituitary) ambapo homoni za FSH, LH na estradiol huwa kwa kiwango cha chini pamoja na kuongezeka au kupungua kwa homoni ya kuzalisha maziwa (Prolactin). (2) Uvimbe kwenye ovari uliojaa maji maji (PCOS); ambao hupelekea hedhi kutokuwa zenye mpangilio, homoni za kiume kuwa nyingi, tatizo hili kufanywa kwa uchunguzi wa picha za miozi (ultrasound). (3) Kasoro zilizopo katika ovari (ambapo homoni ya estradiol huzalishwa katika kiwango cha chini huku FSH kuongezeka katika uzalishaji. Au (4) Kasoro katika tumbo la uzazi
— Uvimbe katika ovari wenye maji maji (Poly cystic ovarian disease); tatizo hili ni kasoro katika ovari (sehemu ya kuzalisha mayai) ambapo hutokea na uvimbe uliojaa maji maji yenye sukari na hupelekea kiwango cha homoni za kiume kuwa kikubwa (hyperandrogenism) pamoja na kiwango cha LH kuongezeka zaidi. Mabadiliko haya ya homoni husababisha changamoto za ukomavu na upevukaji wa mayai na hedhi isioeleweka.
Mtu mwenye tatizo hili la PCOS hukumbwa na changamoto ya kushika ujauzito, mimba kuharibika mara kwa mara, uotaji wa nywele sehemu za usoni - kifuani, uzito usioendana na kimo (uzito mkubwa), changamoto za kisaikolojia zinazotokana na kushindwa kushika ujauzito- muonekano wa kiume usoni na kifuani - na hedhi isiokuwa na mpangilio
PCOS hugundulika kwa kufanya ultrasound - ambayo itaonesha uwepo wa uvimbe na ujazo wa ovari kuwa zaidi ya 10ml. Na kipimo cha homoni hasa LH:FSH ambapo uwiano wake unatakiwa kuwa 1:1 lakini kwa mwenye tatizo hili uwiano wake huwa 2:1 au 3:1 manake kiwango cha LH huzidi kile cha FSH. Lakini hushauriwa kufanya vipimo vya homoni ya kuzalisha maziwa (hyperprolactinemia) ambapo ikiwa nyingi hupelekea mwanamke kujisikia k**a mwenye kunyonyesha au chuchu kuuma, kuvimba na kutoa maziwa au maji maji na huingilia ufanyaji kazi wa homoni za k**e
👉 Magonjwa katika mirija ya uzazi (Tubal disease). Tatizo la PID, matumizi ya uzazi wa mpango wa ndani ukeni, historia ya mimba kutungwa nje ya uzazi, hupelekea mirija ya uzazi kutofanya kazi yake sawa sawa. Kipimo cha Hysterosalpingogram (HSG) au Laparoscopy (kusafishwa mirija) hufanyika mapema kwenye ndoa nyingi.
-- Maambukizi ya bakteria aina ya Chlamydia trachomatis hupuuzwa katika kuchunguzwa kwa undani, hivyo hushauriwa wanandoa wote kutibiwa.
PID ni ugonjwa ambao hutokea sehemu ya uke na uzazi wa mwanamke ambayo huambatana na dalili zifuatazo; (1) Kutokwa na uchafu wenye harufu, uliochanganyika na damu, (2) Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, (3) Maumivu chini ya kitovu, (4) Maumivu ya kiuno, (5) kuwashwa, (6) Kutokwa damu wakati wa tendo, (7) Kukosa hisia ya tendo la ndoa, (8) Maumivu wakati wa kukojoa, (9) Lakini huathiri mzunguko wa hedhi ambapo inaweza kupelekea kutokwa na hedhi isio kawaida. Kumbuka katika ultrasound inaweza kuonesha sehemu ya kizazi ina maji maji yenye bakteria ambayo hudhaniwa kuwa ni uchafu,
👉 Tatizo la tishu/kuta za uzazi kuotea (Endometrosis). Kwa lugha nyepesi ni uwepo wa vinyama vilivyojiotea kwenye kizazi, na uwepo wa hivi vinyama hupelekea kuwa na historia ya kupata maumivu wakati wa ngono (dyspareunia) au maumivu makali ya hedhi (dysmenorrhea). Tatizo hili likiwa la kawaida haliingiliani na upatikanaji wa mimba. Lakini uwepo wa tatizo hili kwa ukubwa husabibisha kasoro katika utengenezaji na upevukaji wa yai, mbegu za kiume kurutubisha yai, na utungwaji wa mimba (mimba kujishikiza katika kuta za uzazi). Endometrosis kitaalamu ni tatizo lililo kimya, ingawa hutolewa kwa njia ya kusafishwa kizazi na mirija yake (laparoscopy)
(4) SABABU ZILIZOPO UPANDE WA MWANAUME
Wanaume nao huwa sehemu ya tatizo la kutoshika mimba kwasababu kuna matatizo mengi ya kiume huhusiana na ugumba kwa mwanamke.
👉Magonjwa yanayohusiana na Korodani na sehemu za kuhifadhia na kusafirisha
👉kasoro au magonjwa katika mfumo wa tezi kuu (hypothalamic - pituitary) ambayo hupelekea kushindwa korodani kufanya kazi yake vizuri
👉Kuna magonjwa ambayo huhusiana na mbegu zenyewe (kasoro katika vinasaba, Y chromosome microdeletions); yawezekana kukosekana (azoospermia) au kiwango kidogo (oligospermia) cha mbegu kwenye shahawa.
-- Kasoro ya kimabadiliko (mutations) katika homoni ya FSH k**a ilivyo kwa wanawake ambavyo kasoro katika FSH hupelekea yai kutokukua na kukomaa hata hivyo kwa wanaume kasoro katika FSH hupelekea uzalishaji mdogo wa mbegu kuwa hafifu zaidi.
-- inakadiriwa kuna 15% za wanaume wenye ugumba unaotokana na shahawa kutokuwa na mbegu na 6% wenye kiwango kidogo cha shahawa.
MATIBABU YA UGUMBA AU KUTOSHIKA UJAUZITO
Ukiacha na athari za uvutaji sigara, pombe, lakini mgonjwa anapaswa kushauriwa juu uzingatifu wa lishe na uzito k**a kiini cha matibabu ya ugumba na ujauzito. Kupungua zaidi au kuwa na uzito zaidi huhusiana na ugumba au ongezeko la athari wakati wa ujauzito
-- Matibabu ya ugumba hupaswa kuangaliwa kulingana na chanzo chake hasa mara baada ya kufanya vipimo. Uzingatifu wa hatua za kimatibabu ni msingi mkuu
👉 Hali ya kuwa na matumaini kwamba kuna kitu kizuri kitakuja kutokea ni msingi wa kisaikolojia kwa wana ndoa.
👉 Kwa tatizo linalohusiana na kasoro za ufanyaji kazi wa ovari zinaweza kutibika kwa; (1) kubadili mtindo wa maisha hasa kwa wanawake wenye uzito mdogo au wenye historia ya kufanya kazi ngumu na mazoezi au uzito mkubwa
- - Matumizi ya dawa zilizopo katika kundi la dopamine agonist (kwa mfano Bromocriptine) zinaweza kutumika kwa wagonjwa wenye kiwango kikubwa cha prolactin homoni
-- Matumizi ya dawa zenye kuongeza ufanyaji kazi wa FSH k**a Clomifene; ni dawa yenye matokeo ya kuongeza upevukaji kwa 60% katika wanawake wenye uvimbe katika ovari. Kumbuka clomifene inaweza kutolewa kwa mwanaume ili kusaidia uzalishaji wa mbegu za kiume
👉 Matibabu ya PCOS; Matibabu bila dawa kwa mwenye changamoto hii ni kwa kufanya yafuatayo. (1) mgonjwa aelezwe chanzo cha tatizo, jinsi tatizo linavoathiri uzazi wake, na jinsi ya kutibu, (2) mgonjwa aelezwe jinsi ya kupunguza uzito kwa kubadili mfumo wa vyakula hasa vyakula vyenye sukari sukari, ufanyaji wa mazoezi
Matibabu kwa kutumia dawa; -changamoto ya hedhi kutokuwa sawa inaweza kuwekwa sawa na moja kati ya dawa zifuatazo; Vidonge vya majira vyenye cyproterone acetate/ co-cyprindiol-dianette ambavyo husaidia kupunguza na homoni za kiume au Norethisterone au Dydrogesterone
- Changamoto ya sukari kuwepo katika ovari hutibiwa kwa kutumia Metformin angalau mwezi mzima
- Changamoto ya yai kutopevuka inaweza kuratibiwa na clomifene
👉 Matibabu ya mfumo wa hedhi huratibiwa kwa kutumia dawa zenye kuongeza homoni mwilini (Hormonal therapy); ambapo dawa huweka katika usawa homoni za hedhi dawa hizo ni k**a Norethisterone, Dydrogesterone (dawa hii hutumika kuweka mfumo wa hedhi sawa, hata kuzuia mimba kuharibika)
👉 Jinsi ya kuhesabu siku za hedhi kwa mtu mwenye siku 28; kwa mfano mwanamke alieingia hedhi tarehe 20/7/2022 hadi 27/7/2022
Siku 10 tangu tarehe ya kuingia hedhi ni salama
—- Kwa mfano wewe hapo tarehe 20/7 hadi 30/7 ulikuwa free ila siku saba ndio ulikuwa hedhi tatu ndio salama (free)
Kuanzia siku ya 11 hadi 20 ni siku ambazo mimba unaweza kushika ambapo siku ya 11 hadi 13 endapo ukifanya ngono isio salama mbegu ya mwanaume huwa hai ndani ya uke hadi siku ya kupevuka yai, siku ya 14 hadi 17 ni hatari zaidi kwasababu yai hupevuka (ovulation period with high chances), siku ya 18 hadi 20 ni siku ambazo yai huwa safarini kuelekea kwenye uzazi na uhatari wa kushika mimba hupungua lakini unaweza kushika ujauzito (low chances)
—— Kwa mfano wewe kulingana na kalenda ya mwezi na mwaka, kuanzia tarehe 31/7 hadi 09/8 ni hatari kwa ujauzito
Kuanzia siku ya 22 hadi 28 yai huwa limeshafika kwenye uzazi na uwezo wake wa kushika mimba hupungua zaidi na ikiwezekana usishike mimba na ni kipindi ambacho humwandaa mwanamke kuingia hedhi
——- kwa mfano wewe hapo kuanzia tarehe 10/8 hadi 17/8 ni siku salama na ambazo zinakutayarisha kuingia hedhi
👉 Tatizo la kuziba mirija hutibiwa kwa kusafishwa sehemu husika
👉 Tatizo la PID hushauriwa kutibiwa kwa aina tatu za dawa; (1) Dawa zenye uwezo katika magonjwa ya zinaa (cover possible gonococcal infection) k**a Ceftriaxone, azithromycin, cefixime, Cefoxitin nk, (2) Doxycycline kwaajili ya bakteria aina ua chlamydial, (3) Dawa zenye kuua bakteria wasiotumia hewa safi wenye tabia ya kuzalisha uchafu, hasa dawa zilizopo katika kundi la Nitroimidazole kwa mfano Metronidazole, Tinidazole, Secnidazole, Ornidazole
Na inashauriwa wanandoa wote kutibiwa ili kupunguza mwendelezo wa bakteria kuwepo na kuathiri, na matibabu haya hushauriwa kufanywa kwa muda wa siku 14
NB: Matibabu mengine yaliainishwa pindi visababishi vikielezwa
ASANTE KWA KUITEMBELEA SANGULAE ONLINE PHARMACY CARE