Elimika NA MONIE

Elimika NA MONIE Ni jukumu langu na najisikia vizuri kuwahudumia wanawake na wanaume wenye changamoto za uzazi.

Unachokihitaji Kuna Mtu anacho Tena hayuko mbali.... Ongea na watu Wana vitu vyako
23/08/2024

Unachokihitaji Kuna Mtu anacho Tena hayuko mbali.... Ongea na watu Wana vitu vyako

03/01/2024
03/01/2024

Vyakula Vinavyoongeza Damu Kwa Wingi Mwilini:*
Vifuatavyo ni vyakula vinavyosaidia kuongeza wingi wa damu katika mwili ambavyo ni pamoja na;

1)MBOGA MBOGA
Mboga za majani k**a vile mchicha, spinach, na kale (leaf cabbage) zina kiwango kikubwa cha folate, madini ya chuma, na vitamini C ambavyo ni muhimu katika uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini.

2) NYAMA NYEKUNDU
Nyama ya ng’ombe, nyama ya kondoo na aina nyingine ya nyama nyekundu ni chanzo muhimu cha madini ya chuma mwilini ambacho ni muhimu katika utengenezaji wa haemoglobini, sehemu ya seli nyekundu za damu.

3)MATUNDA
Matunda k**a vile embe, nanasi, zabibu, chungwa, nyanya yana kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia mwili kuchukua madini ya chuma vizuri zaidi na hivyo kuongeza kiwango cha damu mwilini.

4)JUICE
Sio juisi zote huongeza kiwango cha damu, unashauriwa kunywa juisi ya nyanya, walau kila siku glasi mbili lakini pia juisi za rozella, tikitimaji na karoti. Aina hizi za juisi huongeza kiwango cha damu kuliko hata vidonge.

5.MAHARAGE
Maharage Pia yana kiwango kikubwa Cha madini chuma ambayo huongeza utengenezaji wa seli nyekundu za damu.

''IMARIKA KIAFYA TIMIZA MALENGO YAKO''
2024

16/10/2023

DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

1) KUKOSA HAMMU YA KUFANYA TENDO LA NDOA
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume ni moja wapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume na linaweza kusababishwa na sababu nyingi sana.Sababu hizo zinaweza kuwa za kimaumbile au kisaikolojia au za mchanganyiko zote.Baadhi ya sababu za tatizo hili ni pamoja na;

a) Msongo Wa Mawazo (Depression).

Msongo wa mawazo ni ugonjwa wa kisaikolojia unaohusisha hali ya kuwa na mawazo makali kwa muda mrefu yanapolekea kukosa raha kutokana na kujihisi si mtu wa thamani au kukosa starehe katika vitu ulivyozoea kuvifanya na kukufurahisha hapo awali.Mawazo ya namna hii huathiri mwenendo wako wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukosa matamanio ya kimapenzi.

b) Matumizi Ya Madawa Na Pombe.

Matumizi ya baadhi ya madawa na unywaji wa pombe wa kupindukia vinaweza kupelekea tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.Madawa yanayochangia tatizo hili ni pamoja na;Madawa ya presha ya kupanda(Anti hypertensive drugs), madawa ya kuondoa msongo wa mawazo, madawa yote yanayozuia ufanyaji kazi au uzalishaji wa testosterone, kwa mfano, cimetidine,finasteride na cyproterone n.k

c) Mawazo Mengi Na Uchovu.

Matatizo ya kikazi na hadhi yako kazini vinaweza kuchangia kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.K**a unabezwa sana kazini na kujiona hutimizi kazi yako ipasavyo au k**a unachoka sana kazini pia vinaweza kupelekea kukosa hamu ya kufanya mapenzi pindi urudipo nyumbani kwani mahusiano ya kimapenzi yanahitaji yatengewe muda wa kutosha.

d) Kuwa Na Umri Mkubwa.

Kiwango cha homoni ya testosterone inayohusika na hisia za kimapenzi kwa mwanaume hupungua kwa asilimia 1-2 kila mwaka kadri mwanaume anavyozidi kuwa na umri mkubwa.Kiwango cha testosterone kikishuka katika mwili wa mwanaume humfanya asiwe na nguvu, ashindwe kutuliza mawazo kwenye jambo alifanyalo na apoteze hamu ya kufanya mapenzi.

e) Mahusiano Mabovu Baina Ya Mwanaume Na Mwanamke.

Matatizo ya kimahusiano kati ya mwanaume na mwanamke yana mchango mkubwa sana katika kusababisha tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano uwepo wa migogoro kati ya mume na mke, ukosefu wa amani na furaha katika mahusiano huchangia sana mwanaume kukosa hamu ya kufanya mapenzi.
K**a mahusiano yako na mpenzi wako yamekuwa ya miaka mingi sana, unaweza kuwa umemzoea mno mkeo kiasi kwamba ukaanza kukosa hamu ya kufanya naye tendo la ndoa.Hili nalo hutokea mara nyingi.

f) Matatizo Ya Kiafya.

Matatizo ya kiafya ya muda mrefu(chronic diseases) husababisha kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa, mfano tatizo la kisukari, tatizo la presha, tatizo la moyo, tatizo la kansa ya muda mrefu, bawasiri ,na hali ya kuwa na unene uliozidi kiwango(obesity) n.k

2) KUTOKUWA NA UWEZO WA KURUDIA TENDO LA NDOA ZAIDI YA MARA MBILI
Mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume akishakamilisha mshindo mmoja wa tendo la ndoa basi anakua hana uwezo tena wa kurudia mshindo mwingine.Hali hii husababishwa na kutokuwepo na mshukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume.

3) KUTOKUWA NA UWEZO WA KUSIMAMISHA UUME KABISA AU UUME KUSIMAMA LEGELEGE NA KWA MUDA MFUPI TU

Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika(rijali) unaposimama, hutakiwa kuwa imara k**a msumari, lakini kwa mwanaume mwenye changamoto ya upungufu za nguvu za kiume uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na unaweza kusinyaa wakati wowote.
Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume ambayo ndio huufanya uume usimame barabara.

4) KUWAHI KUFIKA KILELENI CHINI YA DAKIKA 17

Kuwahi kufika kileleni ni hali ambayo inampata mwanaume mwenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambapo hutoa shahawa kabla ya kuanza tendo la ndoa au muda mfupi tu baada ya kuanza tendo la ndoa, bila yeye mwenyewe kukusudia.Kwa kawaida mtu mwenye tatizo la kuwahi kufika kileleni hutoa mbegu zake za kiume hata baada ya maandalizi kidogo sana.

5) KUCHOKA SANA NA KUKINAI KABISA BAADA YA TENDO LA NDOA WAKATI MWINGINE KUSIKIA HADI KICHEFUCHEFU

Hii ni mojawapo ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume.Hali hii huwapata wanaume wenye changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume ambayo wakati mwingine huambatana na usingizi mzito(Kulala fofofo).

6) KUHISI MAUMIVU WAKATI/BAADA YA TENDO LA NDOA

Hii pia ni mojawapo pia ya dalili za upungufu wa nguvu za kiume, hali hii huweza kuchangiwa na kauthirika kwa tishu za uume ambazo hutokana na upigaji wa punyeto kupita kiasi.

7) KUCHELEWA/KUSHINDWA KABISA KUFIKA KILELENI

Ni ile hali ya mwanaume kuchukua muda mrefu kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa kawaida mwanaume anatakiwa afike kileleni/kutoa manii kwa muda usiozidi dakika 30 wakati wa kushiriki tendo la ndoa.Kwa hiyo mwanaume anaposhiriki tendo la ndoa na kuchukua muda mrefu bila kufika kileleni anahitaji uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo.

08/10/2023

*UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NINI??*

Upungufu wa Nguvu za Kiume *Ni hali ya kushindwa kufanya mapenzi kikamililifu au kushindwa kusimamisha vizuri na kushindwa kutungisha Mimba.* Shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu.

*Tatizo hili huripotiwa kuwa katika wanaume watatu (3) basi mmoja kati yao anatatizo la upungufu wa nguvu za kiume.* Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kuto kuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.

*Hili tatizo huwanyima watu raha kwa kuwa na mawazo, kuwa na matatizo katika mahusiano. Watu wengi wenye tatizo hili wanahitaji kutumia dawa zisizo na madhara na kubadilisha mitindo ya maisha yao ili kuweza kurudisha hali zao na kuondoa tatizo, cha msingi ni kuzingatia yale utakayoelekezwa.*

Kuna matatizo ya kutofanya mapenzi kikamilifu, nayo ni; kuwahi kumwanga mbegu za uzazi, Kuto kumwaga, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa.

*Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume pia.

Send a message to learn more

28/09/2023

JINSI YA KUPONA TATIZO LA TEZI DUME BILA UPASUAJI KWA MIEZI MITATU TU

Je, wewe ni mwanaumea uliyehangaika kwa muda mrefu kutatua changamoto ya kuvimba kwa tezi dume hali ambayo imepelekea kukojoa damu kila wakati,kushindwa kukojoa na kuwekewa mpira wa mkojo muda wote,kushindwa kumudu tendo la ndoa kwa kuishiwa nguvu za kiume na kupelekea ugomvi kwenye ndoa yako,Kushindwa kuzuia mkojo na kujikuta umejikojolea

K**a jibu ni ndiyo usiwaze maana leo nimekuletea suluhisho la changamoto yako,inawezekana habari hii inaenda kurejessha tabasamu kwenye afya yako.

Huhitaji kufanyiwa upasuaji na kutumia dawa za kemikali kutatua changamoto yako ya tezi dume,tiba halisi ipo kwenye virutubisho asili vilivyotengenezwa kwa mimea na matunda ambavyo vinaenda kufanya maajabu yafuatayo;-

1.Kuondoa tezi dume bila upasuaji

2.Kuzuia kuvimba kwa tezi dume

3.Kuzuia na kukimga matatizo ya mkojo kwa mwanaume.

4.Kusaidia na kuongeza uzalishwaji wa mbegu za kiume.

5.Kuboresha na kukinga figo isipate madhara.

6.Kuzuia na kukinga kusambaa kwa kansa.

7.Kuongeza kinga ya mwili na kuzalisha seli mwilini.

8.Kubalance homoni za kiume.

Huduma zetu zinakufikia mahali popote ulipo BURE kabisa.

Kwa ushauri na tiba karibu sana.

Thamani ya virutubisho. 0789907021

20/09/2023

*HABARI ZA WAKATI HUU??*

LEO KWENU WANAUME WOTE KWA PAMOJA TUNAWALETEA NAKALA NZURI NA MUHIMU ZAIDI KUHUSU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

*TUTAJIKITA ZAIDI KUHUSU👇👇;*
1.MAANA UA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME KWA UJUMLA WAKE.
2. VYANZO VYA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
3. DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
4. HASARA(MADHARA YA) ZA KUPUNGUA KWA NGUVU ZA KIUME
5. TIBA YA KUDUMU INAYOTOKOMEZA TATIZO SUGU LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

*FATANA NASI HATUA KWA HATUA.

21/08/2023

KUVURUGIKA KWA HOMONI KWA MWANAMKE [HORMONAL IMBALANCE]

HOMONI ni kemikali zenye nguvu ndani ya mwili zinazozalishwa na matezi, homoni ndizo humfanya mwanaume kuwa mwanaume na mwanamke kuwa mwanamke mf. ndevu,bass, sauti nyororoo, ngozi laini n.k

HOMONI zinapozidi au kupungua huathiri mwili kwa kiwango cha juu sana.

**DALILI ZA KUVURUGIKA KWA HOMONI**

1.Kutokushika mimba

2.Kutoka na hedhi nzito au kukosa hedhi kwa miezi kadhaa,hedhi kuruka,kutoka hedhi mfululizo

3.Kutoka chunusi usoni,kifuani na mgongoni kwa juu

4.Kupata maotea ya ngozi [skin tags]

5.Uke kuwa mkavu

6.Maumivu wakati wa tendo la ndoa

7.Maumivu ya kiuno, mgongo na tumbo chini ya kitovu

8.Maumivu ya kichwa mara kwa mara

SABABU ZINAZOPELEKEA KUVURUGIKA KWA HOMONI

1.Matumizi ya njia za uzazi wa mpango k**a sindano na vidonge .

2.Stress/msongo wa mawazo.

3.Ulaji mbovu

4.Matumizi ya tiba za kansa k**a vile mionzi

5.Kisukari

6.Goita

7. Ujauzito na kunyonyesha.

MADHARA YA KUVURUGIKA KWA HOMONI KWA MWANAMKE
1. Kutokushika mimba
2.Mimba kutoka mara kwa mara
3.Kuvurugika kwa hedhi
4.Kukaribisha magonjwa katika mfumo wa uzazi

MATIBABU
Namna ya kutatua tatizo la Kuvurugika kwa homoni kwa kutumia virutubisho lishe wasiliana nasi kwa Whatsapp namba 0789907021.

JINSI YA KUONDOKANA NA TATIZO LA FANGASI SUGU AU INAYOJIRUDIARUDIA UKENI.Je,umekuwa umekuwa ukitamani kuwa na uke wenye ...
14/08/2023

JINSI YA KUONDOKANA NA TATIZO LA FANGASI SUGU AU INAYOJIRUDIARUDIA UKENI.

Je,umekuwa umekuwa ukitamani kuwa na uke wenye afya bora, jambo ambalo litakuongezea kujiamini na kuwa na furaha kwenye ndoa/mahusiano yako?.

Naelewa changamoto yako na niko tayari kukusaidia.

Nimeandaa darasa BURE litakalokusaidia kuondokana na changamoto yako .

Kwenye darasa hili nitakufundisha njia rahisi za kuondokana/kujikinga na tatizo la fangas sugu na inayojirudiarudia ukeni.

Kupata darasa hili bofya neno Whatsapp hapo chini kisha tuma jina lako nikuunge kwenye group.

12/08/2023

MAMBO YA KUZINGATIA KWA MWANAMKE ILI KUWEKA UKE KATIKA HALI YA USAFI NA AFYA BORA

Uke wenye afya bora ni fahari kwa mwanamke na furaha kwa mume/mwenzi wake.Uke wenye Afya bora utakufanya mwanamke ujiamini na kujithamini.
Kutokwa na uchafu na wenye harufu mbaya inaashiria kuwa hauko sawa kiafya na ni kwamba unaumwa.

Leo twende tuone mambo muhimu saba 7 ambayo ukiyazingatia utakuwa na uke safi na wenye afya bora kabisa ;

1.Epuka kujisafisha kwa kuingiza kidole ndani [Vaginal douching]
Wapo wanawake wengine husafisha uke kila mara hasa kwa kutumia kemikali, sabuni na kwa kuingiza kidole ndani ya uke.Njia hii ya kujisafisha haishauriwi kabsa kiafya kwani huondoa na kuharibu bakteria wazuri ukeni [Normal flora]. Bakteria hawa ni walinzi kwenye uke hivyo unapowaharibu unaacha nafasi kwa uke kushambuliwa na bakteria wabaya,fangasi pamoja na candida na kupelekea kupata magonjwa ukeni.

Badala yake unashauriwa kujisafisha kwa maji na sabuni ya kawaida tu isiyo na kemikali na kwa juu bila kuingiza kidole ndani maana uke hukosafosha wenyewe katika hali ya kawaida.

2.Jitawaze kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kutoka haja ndogo au kubwa.
Hakikisha unanawa na maji safi kila baada ya haja kubwa au ndogo. Nawa kwanza mbele [ukeni] ukishamaliza ndipo unawe nyuma [sehemu ya haja kubwa] ili usieneze bakteria wanaotoka kwenye njia ya haja kubwa kuja ukeni maana utajiletea maambukizi.

3. Vaa nguo za ndani za pamba na zisizobana.
Nguo za ndani za nailoni na zinazobana Zinazuia hrwa safi kupita kuelekea ukeni hivyo kusababisha unyevunyevu ambao ndio mbolea kwa bakteria na fangus wabaya wanaoleta harufu mbaya ukeni.Na pia hakikisha unabadilisha nguo ya ndani kila baada ya masaa 12 ili kusaidia kuzuia ukuaji wa fangasi na bakteria wabaya ukeni.

4.Epuka baadhi ya vyakula ambavyo ni adui kwa afya ya uke.
Kuna baadhi ya vyakula sio rafki kwa afya ya uzazi wa mwanamke kwani vinaharibu afya ya uke na kuua bakteria walinzi[normal flora] na kubadili pH ya uke. Vyakula hivyo ni pamoja na vyakula vya sukari, pombe, vyakula vilivyosindikwa kwani huchochea ukuaji wa fangas [candida].

5.Badili nguo zako za ndani kila baada ya kufanya mazoezi au mwendo mrefu.
Badili nguo zako za ndani zenye unyevunyevu kila baada ya kufanya mazoezi au mwendo mrefu bila kukawia kwani nguo zenye unyevunyevu ni mbolea nzuri kwa ukuaji wa bakteria wabaya,hii itakusaidia kuwa na uke wenye afya.

6.Epuka kutumia spray au marashi ukeni.
Ngozi ya uke kwa kawaida ni laini sana hivyo hunyonya kemikali zilizoko kwenye marashi kiurahisi zaidi na kuingia kwenye damu.Uke wenye afya hauhitaji spray wala marashi.

7. Punguza uzito k**a inawezekana.
Uzito mkubwa na kitambi vinakufanya utokwe na jasho kwa wingi zaidi hasa kwenye uke ambapo jasho na unyevunyevu vinaleta fangas na bakteria wabaya.Hivyo chagua kula lishe nzuri ,pua fanya mazoezi ili kurekebisha mwili wako.

Address

Shinyanga

Opening Hours

Monday 09:00 - 22:00
Tuesday 09:00 - 22:00
Wednesday 09:00 - 22:00
Thursday 09:00 - 22:00
Friday 09:00 - 22:00
Saturday 09:00 - 22:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elimika NA MONIE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Elimika NA MONIE:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram