Al-Madrasat Tan-Mbihi Shinyanga

Al-Madrasat Tan-Mbihi Shinyanga Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Al-Madrasat Tan-Mbihi Shinyanga, Massage service, 492, Shinyanga.

Jumaa Mubaaraka
03/12/2021

Jumaa Mubaaraka

Shekh Wa Mkoa wa Shinyanga Istiqama Sunni waljamaa Tanzania (Isuwat), SHKH MAULID ABDALLAH Amepokea kwa masikitiko makub...
24/05/2021

Shekh Wa Mkoa wa Shinyanga Istiqama Sunni waljamaa Tanzania (Isuwat), SHKH MAULID ABDALLAH Amepokea kwa masikitiko makubwa kifo Cha aliekuwa katibu wa Mtaa wa M***i Issa Shaaban Simba (BAKWATA) Ndg Ibrahimu Mitiliga, hivyo anatoa pole kwa Baraza kuu na Shekh Wa Mtaa wa M***i Simba pamoja na waislam woote kwa ujumla Allah atufanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu Cha kutokewa na kipenz chetu Aamin
INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAJIUN

Uongoz mzima wa Almadrasat Tanmbihi unawatakia Waislamu kote Nchini Tanzania na nje ya mipaka; Heri ya Sikukuu ya Eid Al...
24/05/2020

Uongoz mzima wa Almadrasat Tanmbihi unawatakia Waislamu kote Nchini Tanzania na nje ya mipaka; Heri ya Sikukuu ya Eid Al Fitr 🇹🇿🙏🏽🙏🏽

20/05/2020

Shekh Wa mkoa Shinyanga Istiqama na mudiru wa Almadrasat Tanmbihi akizungumzia Mambo aliyokuwa akifanya mtume katika kumi la mwisho ndan ya Ramadhan

Share na comment ili tuwaidhike sote inshallah

KWELI DUNIA DUARA1. NIKABU AMBAYO IMEKUWA IKIONEKANA INAMNYIMA UHURU MWANAMKE WA KIISLAM NAKUONESHA KUWA MTU AKIVAA HAWE...
30/04/2020

KWELI DUNIA DUARA

1. NIKABU AMBAYO IMEKUWA IKIONEKANA INAMNYIMA UHURU MWANAMKE WA KIISLAM NAKUONESHA KUWA MTU AKIVAA HAWEZI KUPUMUA VIZUR NA KUONESHWA HAIFAI KTK MAENEO FULANI NA KUWASHURUTISHA WAZIVUE, LEO HII HATA ISOWAHUSU WAIVAA NA AJABU ZAIDI MPAKA WANAUME WAIVAA KWA JINA LA BARAKOA.

2. WAZUNGU WANATAMANI WAJE KUWA WAKIMBIZI AFRIKA WAKATI WAO WAMEKUWA HAWAWATAKI WAAFRIKA WANAOKIMBILIA KWAO.

3. UISLAM UNAMKATAZA MWANAMNE NA MWANAMKE AMBAO WANAWEZA KUOWANA KUPEANA MIKONO. HII IMEKUWA IKIONEKANA KWAMBA UISLAM NI DINI YA KIBAGUZI NA HILI HALIWEZEKANI. JE, CORONA IMEWEZESHA AU HAIJAWEZESHA?

4. TUNAPOTAWADHA MARA TANO KWA SIKU KWA AJILI YA SWALA AU KUNAWA MIKONO KWA AJILI YA CHAKULA UISLAMU UNASISITIZA KUTUMIA MAJI YANAYOTIRIRIKA. LEO TUNAAMBIWA TUNAWE KWA SABUNI NA MAJI YANAYOTIRIKA IKIWA NI MOJA YA NJIA ZA KUJIKINGA NA CORONA. MTUME MUHAMMAD ALISHAFUNDISHA HAYA YOTE KARNE NYINGI ZILIZOPITA KABLA YA SAYANSI YA KILEO.

5. UISLAM UNASISITIZA KWAMBA BINADAMU WOTE NI SAWA NA ALIYE BORA MBELE YA MWENYEZI MUNGU NI MCHAMUNGU TU. LEO HII CORONA IMETHIBITISHA KWAMBA BINADAMU WOTE NI SAWA KWANI IMEWAPATA TAKRIBANI WATU WA MATAIFA YOTE BILA KUJALI TAJIRI, MASIKINI, SUPER POWER AU MINOR POWER, MZUNGU, MWARABU AU MWAFRIKA. WOTE NI KILIO CHA CORONA.

6. KUHUSU KATANTINI MTUME MUHAMMAD ALISEMA KWAMBA KUNAPOKUWEPO NA MARADHI YA MLIPUKO SEHEMU FULANI BASI WALIOPO ENEO HILO WASITOKE ILI WASIWAAMBUKIZE WENGINE NA WALIO NJE YA ENEO HILO WASIINGIE KWENYE ENEO LENYE MLIPUKO ILI WASIJE KUAMBUKIZWA NA KUENDELEA KUSAMBAZIANA.

7. NDANI YA QUR'AN ALLAH ANASEMA KWAMBA WAKATI WA SHIDA HATA ANAYEKANA NA KUTOAMINI UWEPO WA MUNGU NDIO HUMKUMBUKA NA KUMTAJA MUNGU. CORONA IMETHIBITISHA HILO KWANI HIVI SASA KILA TAIFA NA KILA KINYWA NA BINADAMU KINAMTAJA MWENYEZI MUNGU.

8. MTUME MUHAMMAD ANASEMA KWAMBA MMOJA WENU ANAPOTOKA KUAMKA BASI ASISHIKE AU KUINGIZA MIKONO KWENYE CHOMBO AU SEHEMU SAFI MPAKA ANAWE PEMBENI KWA MAJI YANAYOTIRIRIKA MARA TATU KISHA NDIO AINGIZE AU ASHIKE. LEO TUNASISITIZWA KUTOSHIKA MACHONI, PUANI AU MDOMONI KWA MKONO HUENDA UKABEBA VIRUS WA CORONA NA KUJIAMBUKIZA. MAFUNDISHO YA UISLAMU ULISHAFUNDISHA HAYO TANGU KARNE NYINGI ZILIZOPITA.

9. MTUME MUHAMMAD AMESEMA UNAPOPIGA CHAFYA AU MIAYO UNATAKIWA UZIBE KWA MDOMO NA LEO HII IMEKUWA NI MOJA KATI YA TAHADHARI ZA KUJIKINGA NA KUWAKINGA WENGINE DHIDI YA CORONA.

HAKIKA UISLAMU UNA MENGI MNO YANAYOENDANA NA MAUMBILE NA MAISHA HALISI YA VIUMBE WOTE KWA KUJALI AFYA NA HALI YA KILA KIUMBE.

ASILI YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAARIFA YA ELIMU NA FANI ZOTE KTK DUNIA HII HUPATIKANA NDANI YA QURAN NA MAFUNDISHO YA MTUME MUHAMMAD KWA UJUMLA.

ANAYEUKATAA UISLAMU NA AUKATAE KWA JEURI YAKE NA KUTOKANA NA KUTOTUMIA AKILI YAKE VIZURI.

HAKIKA UISLAM NDIO DINI YA HAKIKA WASHIRIKA WENGINE WA PROPAGANDA CHAFU DHIDI YA UISLAM WANALIJUA HILO NA HUFANYA VITA DHIDI YA UISLAMU NA WAISLAMU KWA MAKUSUDI. SASA ALLAH AMEAMUA KUDHIHIRISHA YEYE MWENYEWE UKWELI WA UISLAMU.

Share ili umma uwaidhike

19/09/2019

Aliamka asubuhi lakini alishangaa kuuona mwili wake bado upo kitandani ukiwa umelala, alishtuka na kushindwa kuelewa ni nini kimemtokea, alimwangalia mwanafunzi mwenzake wanaye lala naye chumba kimoja lakini bado alikuwa amelala, alianza kumuita ili amshirikishe kilichomtokea lakini rafiki yake yule hakuweza kuisikia sauti yake, akaamua kumsogelea ili kumtingisha lakini hakuweza kumgusa,, nafsi ile ilianza kuingiwa na wasiwasi na kuamua kutoka nje ya geti lakini alishangaa pia kupita tu bila kufungua mlango,
Alizidi kuchanganyikiwa lakini hakuwa na jinsi aliamua kurudi katika chumba chake lakini chakushangaza aliwakuta marafiki wenzake wakilia na kusema "jesca hatupo nae tena" daaah!! Baada ya kusikia hivyo aliishiwa guvu zote alijitaidi kusema jambo lakini hakuweza kusikika, akawaza na kusema "mbona nimeondoka gafla hivyo sijaweza hata kujiandaa je! Nafsi yangu itaenda kukaa wapi sasa?"

Ni maneno yalio tolewa na nafsi yenye manung'uniko.
Ndugu yangu wewe bado unanafasi basi anza sasa kujisafisha na kujiandaa ili nafsi yako ije ikae mahala pema na pakutulia. Share ujumbe huu kadri uwezavyo k**a Mimi nilivyo share na wewe pia usisahau
KULIKE PAGE HII

Ubora wa Tan-mbihi haujawahi kushuka.Unaikubali kauli hii kwa asilimia ngapi ???
17/08/2019

Ubora wa Tan-mbihi haujawahi kushuka.
Unaikubali kauli hii kwa asilimia ngapi ???

21/02/2019

Usikose usiku wa 16-03-2019 Tan-mbihi Shinyanga

🌹 *_MWALIKO WA MAULID_*🌹              Assalam alaykumShekh mkuu wa Almadrasat *TAN-MBIHI SHINYANGA _SHEKH MAULID ABDALLA...
10/02/2019

🌹 *_MWALIKO WA MAULID_*🌹
Assalam alaykum
Shekh mkuu wa Almadrasat *TAN-MBIHI SHINYANGA _SHEKH MAULID ABDALLAH_* Anayofuraha na heshima kubwa kukualikeni nyote vipenzi wa mtume wetu _Muhammad swalla llahu alayhi wasallama_ kuhudhuria katika maulidi kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa *Almadrasat TANMBIHI NDALA SHINYANGA* tarehe *16-03-2019* kuanzia saa mbili kamili usiku,
pia kuanzia saa *tisa alasiri* kutakuwa na *Dua* kubwa ya kurehemu mashekh zetu mbalimbali waliotangulia mbele ya haqqi pamoja na ndg na jamaa zetu

*Nyote mwakaribishwa*

Imetolewa: Idara ya habar & mawasiliano
*Almadrasat Tan-mbihi Shinyanga*

SHEKH MAULID ABDALLAH (MD)Akifikisha jambo katika hadhwara leo akiwa mgeni rasmi
16/09/2018

SHEKH MAULID ABDALLAH (MD)
Akifikisha jambo katika hadhwara leo akiwa mgeni rasmi

14/09/2018

Maadhimisho ya mwaka mpya wa kiislam 1440 Shinyanga

20/07/2018

بسم الله الرحمن الرحيم.

HUYU NI MWANADAMU

Mwanadamu ni kiumbe dhaifu hata akimiliki mali nyingi na vyeo au uzuri.

وَخُلِقَ الإِنسانُ ضَعيفًا

Na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.(Annisaai 28)

Miongoni mwa udhaifu wa mwanadamu na ndiyo sababu kubwa ya kuharibikiwa ni kuyaendea mambo kwa pupa pasi na kutafakari mwisho wake.

وَيَدعُ الإِنسانُ بِالشَّرِّ دُعاءَهُ بِالخَيرِ ۖ وَكانَ الإِنسانُ عَجولًا

Na mwanaadamu huomba shari k**a vile aombavyo kheri, kwani mwanaadamu ni mwenye pupa (Al israai 11)

Akikosea hajui k**a kakosea hujiona anatengeneza na akikosolewa anaghadhibika.

وَإِذا قيلَ لَهُم لا تُفسِدوا فِي الأَرضِ قالوا إِنَّما نَحنُ مُصلِحونَ

Na wanapo ambiwa: Musifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji (Albaqara 11).

Hakika kila mwanadamu anapo haribu asidhani kwamba jamii yote itamuona anaharibu bali wapo watakao mshangilia na kumuunga mkono kwa kumuona akatengeneza.

Haribu pesa kwa ulevi kuna baadhi watakwazika na hali hiyo lakini utapata marafiki wa kulewa nao na watakupenda na kukushangilia hata siku moja hawatokuambia unaharibu bali watakutukuza na kukupamba.

Hivyo ndivyo walivyo Wanadamu, ukiwasikiliza umeangamia.

والله أعلم.

Address

492
Shinyanga

Telephone

0764177747

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Al-Madrasat Tan-Mbihi Shinyanga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram