DR BWIRE Healthy Service

DR BWIRE Healthy Service Ukurasa huu ni maalumu kwa ajili ya Kuelimisha jamii juu ya magonjwa ambukizi/yasiyoambukiza na tiba

SABABU KWANINI MWANAMKE ANATOKWA NA MAZIWA BILA MIMBAKuongezeka kwa homoni ya PROLACTIN kwa mwanamke sio ishara njema kw...
25/02/2025

SABABU KWANINI MWANAMKE ANATOKWA NA MAZIWA BILA MIMBA

Kuongezeka kwa homoni ya PROLACTIN kwa mwanamke sio ishara njema kwasababu inaweza kusababisha mwanamke kutokwa na maziwa kwenye matiti na endapo tatizo hilo lisiposhuhulikiwa kwa haraka basi linaweza kusababisha ugumba



Homoni ya PROLACTIN kwa mwanamke inasaidia Kukuza matiti wakati wa mimba na kuzalisha maziwa baada ya mwanamke kujifungua wakati wa kunyonyesha.



Lakini homoni hiyo inapoongezeka na kupanda wakati mwanamke hayupo kwenye hali hizo mbili yani hali ya ujauzito au kunyonyesha, inaashiria mwanamke huyo ana ugonjwa unaoitwa HYPERPROLACTINEMIA.
Kwa mwanamke HYPERPROLACTINEMIA inaweza kusababisha:

Mwanamke kupata maumivu makali wakati wa hedhi
Dalili mbaya kwa mwanamke kabla ya hedhi na wakati wa hedhi k**a vile kuharisha, kutapika, maumivu ya mgongo na kichwa.
Mwanamke kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi

Mwanamke kuingia hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi

Mwanamke kuota ndevu kifuani na chini ya kidevu.

Mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa
Mwanamke kuwa mkavu sana wakati wa tendo la ndoa.

Chuchu za mwanamke kutoa maziwa bila kuwa na ujauzito au kunyonyesha

MAMBO YANAYOSABABISHA PROLACTIN KUPANDA NA KUWA JUU.

KITAMBI NA UZITO MKUBWA
Kadri hazina ya mafuta inavyo ongezeka mwilini kutokana na kitambi na uzito mkubwa, ndivyo uzalishaji wa homoni ya Estrogen kutoka kwenye seli zinazo hifadhi mafuta kuongezeka na kuchochea homoni ya PROLACTIN kupanda na kuwa juu.

Magonjwa ya Tezi ya Thyroid.
Hili linatokea endapo tezi ya shingo ikianza kuzalisha homoni chini ya kiwango salama kwa sababu ya maradhi k**a Hashimoto ambayo yanapelekea kinga zako za Mwili kuishambulia Tezi ya Thyroid. Mashambulizi haya hupelekea Tezi ya Thyroid kuzalisha kiwango kidogo cha Homoni zake.

Mwanamke Kutokupevusha Yai.
Mwanamke anaweza kuingia hedhi lakini Yai linakua halijapevuka, hivyo kitendo cha yai kutokupevuka inapelekea homoni ya GONADOTROPIN kutemwa kwa wingi na kusababisha kupanda kwa homoni ya PROLACTIN.

Maradhi ya Kisukari
Hali ya mwili kuwa katika msongo wa homoni ya Insulin nyingi muda wowote kwenye mwili wa mwanamke hupelekea kuvuruga kwa homoni za mvurugiko wa hedhi.

Mazoezi magumu ya kimashindano, hupelekea uzalishaji wa homoni ya PROLACTIN kwasababu ya msongo mkali wa mashindano hayo.
Vyakula hasa vya wanga na sukari. Tafiti zinaonesha kwamba kiwango cha Prolactin hupanda kwenye damu kutokana na kuathiriwa kwa homoni inayotolewa na utumbo mwembamba inayoitwa Vasoactive Intestinal Peptide (VIP) kupanda.
Homoni hii inawatesa wanawake wengi kwasababu inawakosesha hamu ya tendo la ndoa.

Dr BWIRE healthy services Tupo kwa ajili yako,
Ndgu zangu Nina ombi Moja kwenu Nina ndgu yangu ni Mlemavu anajishughulisha na uandishi wa mashairi na Ameingia kwenye kinyang'anyiro Cha kuwania tuzo ya Mashairi Bora wa mwaka hivo k**a hutojali nisiaidie Kumpigia kura Na utakuwa umeniunga mkono kwa asilimia kubwa Yeye anaitwa JANE DAVID ni mgombea namba 0013 kumpigia kura kwa upendo wako Tumia link hii hapa chini ahsante sana 🫶🫶

https://www.facebook.com/share/p/15JhhPqFwW/

Hello wanafamilia wa Facebook, Dr BWIRE Niko hapa kwa Jambo Moja tu Leo hii.Nina Rafiki yangu kipenzi, Nimesoma nae Chuo...
23/02/2025

Hello wanafamilia wa Facebook, Dr BWIRE Niko hapa kwa Jambo Moja tu Leo hii.

Nina Rafiki yangu kipenzi, Nimesoma nae Chuo Cha afya lakn anajishughulisha na uandishi wa mashairi na Ameingia kwenye kinyang'anyiro Cha kuwania tuzo ya Mashairi Bora kipengele Cha mashairi Bora wa mwaka.

Sio kazi sana bonyeza link hapo chini halafu mpigie kura jina lake ni JANE DAVID
Oyaaa mwanangu eeeee utakuwa umetisha sana 👊👊👊

https://www.facebook.com/share/p/15JhhPqFwW/

EID MUBARAKA
11/04/2024

EID MUBARAKA

UGONJWA WA GENITAL-WARTS (Masundosundo) Ge***al warts au kiswahili Masundosundo huu ni ugonjwa unaoota vinyama vidogo kw...
12/10/2023

UGONJWA WA GENITAL-WARTS (Masundosundo)

Ge***al warts au kiswahili Masundosundo huu ni ugonjwa unaoota vinyama vidogo kwenye ngozi au utando laini una zunguka maeneo ya siri.vinyama hivi huweza kuota kwenye uume,uke,mrija wa mkojo,shingi y kizazi kwa wanawake au maeneo kuzunguka haja kubwa au ndani yake.Ugonjwa huu ni miongoni mwa maginjwa ya zinaaa.

CHANZO CHA MASUNDOSUNDO
Ugonjwa huu husababishwa na virusi wanaoitwa Human papilloma Virus (HPV).Kuna aina nyingi za Hpv aina zaid ya 70 ingawa si wote husababisha ugonjwa huu.Baadhi ya Hpv husababisha masundosundo kwenye mikono na miguu. Hpv pia huweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kw wanawake na saratani ya njia y haja kubwa kwa jinsia zote.

UENEAJI WA MASUNDOSUNDO
Ugonjwa huu k**a magonjwa mengine ya zinaa huenea kwa njia ya KUJAMIIANA (Ngono).
Mara baada ya kuambukizwa Hpv huchukua wiki 6 hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri ingawa baadhi huchukua hata miaka kadhaa.

DALILI ZA MASUNDOSUND0
1-kuota kinyama laini juu ya ngozi ingawa muda nwingine huwa vidogo kiasi cha kutoonekana.
2-kwa wanaume hutokeza katika ngozi ya korodani,eneo la mitoki,mapajani,eneo la kuzunguka haja kubwa au ndani yake. 3-kwa wanawake ndani ya uke,njia ya haja kubwa,nje ya uke,eneo la kuzunguka shingo ya kizazi.

NJIA ZA KUJIKINGA NA MASUND0SUNDO
1-Kuepuka ngono (kinyume na maumbile)
2-Kufanya ngono salama
3-kuwa na mwaminifu katika ndoa yako
4-Kuepuka kuvaliana nquo za ndani

UCHUNGUZI WA KIMAABARA
Kwa wanawake uchunguzi hujumuisha maeneo ya nyonga ambapo daktari huchunguza eneo hilo kutumia kifaa maalumu kitakacho msaidia kuona masundosundo.
Pia kipimo cha Pap smear kwa ajili ya uchunguzi wa shingo ya kizazi.
Kwa wanaume ni uchunguzi wa sehem za siri kubaini ugonjwa huu
MATIBABU YA MASUNDOSUNDO
Ni vizuri kutibiwa na daktari akiwa amethibitisha uwepo wa tatizo hili kwa vile kunauwezekano wa kuchanganya baadhi ya aina za dawa nyingine za warts.

NB:MATIBABU YA MASUNDOSUNDO K**A YALIVYO MATIBABU MENGINE YA NJIA ZA NGONO NI LAZIMA YAHUSISHE PIA TIBA KWA MWENZI WA MGONJWA.
DR BWIRE Healthy Service Your Healthy Our preority

UTANGOTANGO👉Ugonjwa huu unasababishwa na maambukizi ya fangasi. Vijana na watu wazima mara nyingi ndio wanaoathirika, pi...
17/06/2023

UTANGOTANGO

👉Ugonjwa huu unasababishwa na maambukizi ya fangasi. Vijana na watu wazima mara nyingi ndio wanaoathirika, pia mara kadhaa hutokea kwa watoto. Fangasi hawa wanakula mafuta yanayotolewa kwenye mwili wa binadamu.
👉Mazingira ya joto pamoja na unyenyevu yanafanya ugonjwa huu kuamka. Ugonjwa huu hautokani na uchafu,pia hauambukizwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Kwa watu wazima mara nyingi unatokea kwenye mwili wakati kwa watoto huwa unatokea usoni.

MATIBABU
👉Mgonjwa anahitaji kutumia dawa za fangasi za kupaka kwa muda wa wiki 2 hadi 3. Baada ya kupaka dawa kwa muda huo rangi ya ngozi inaweza kuchelewa kurudia hali ya kawaida na wakati mwingine hata baada ya miezi kadhaa.

ONYO: USITUMIE MAFUTA YA BREKI NI HATARI

K**a umefaidika na Elimu hii ya Bure kabsa tunaomba usambaze pia usisahau kutufollow na kulike pia AHSANTE 🤝

Kwa changamoto yeyote wasiliana na Daktari
WhatsApp:0685184000
DR BWIRE Healthy Service YOUR HEALTHY OUR PREORITY

Hii miongoni mwa visababishi ni utumiaji wa antibiotics Bila UTARATIBU kwa wajawazito *Nitoe wito unapojihisi ni mjamzit...
11/06/2023

Hii miongoni mwa visababishi ni utumiaji wa antibiotics Bila UTARATIBU kwa wajawazito *Nitoe wito unapojihisi ni mjamzito au unapohisi mkeo ni mjamzito anapopata/kuhisi hali ya ugonjwa unashauriwa KUFIKA kituo Cha Afya mara Moja kabla hunatumia dawa yeyote* 🤝

MWANAUME LAZIMA USOME HII 📌💨 Wiki iliyopita nikiwa kwenye majukumu ya kila siku kwenye wadi ya dharura, ghafla nikakutan...
10/06/2023

MWANAUME LAZIMA USOME HII 📌

💨 Wiki iliyopita nikiwa kwenye majukumu ya kila siku kwenye wadi ya dharura, ghafla nikakutana na kijana mdogo umri wake ni k**a miaka 17 hivi ambaye alikuwa akilalamika kuwa na maumivu ya korodani ya kushoto kwa muda wa takribani siku tatu. Maumivu yalikuwa makali lakini alidharau na kuamini kuwa yataisha muda si mrefu😔 Maumivu yalipozidi akaenda kituo cha kutolea huduma za afya ambako alipewa 'antibiotics'⚕️. Pengine walidhani kuwa ana 'orchitis' au "kipumbu" k**a waitavyo Waswahili. Ikaja kugundulika baadaye kuwa ana tatizo linaloitwa "msokoto wa korodani" huko uzunguni wanaita 'Testicular Torsion'.
Masikini kijana huyu, wakati akiingia kwenye Hospitali niliyokuwepo tayari alikuwa kachelewa🤦🏾‍♂️. Damu ilikwisha kata mzunguko wake kwenye korodani ya kushoto muda mrefu sana na seli huko zimekwisha kufa kitambo! Namna pekee ya kumsaidia kijana huyu ni kuitoa korodani nje! 💔
Jambo la kushukuru Mungu ni kuwa ilikuwa korodani moja tu ya upande wa kushoto na si zote mbili🤲🏾, K**a ingekuwa zote mbili basi bwana mdogo asingeweza kupata mtoto kabisa na mipango yake ya baadaye ingekuwa ghafla imeyeyuka 😢
💨Nasimulia story hii nikiwa naamini kwamba watu wengi hawana uelewa kabisa na tatizo hili. Kisa hiki si cha kwanza kukutana nacho, nimepata kukutana na kisa cha mtu mwingine aliyekuwa na miaka kati ya 30-35 ambaye tatizo lilimpata kwenye korodani zote mbili😢

📌📌 TESTICULAR TORSION (TT) au MSOKOTO WA KORODANI ni tatizo linalotokea pale mrija wa mbegu za kiume ulioshikilia mishipa ya damu unapojikunja na kujisokota kiasi cha kupelekea mishipa ya damu kukunjika na kutopitisha damu kwa ufanisi. Hali hii husababisha tishu zilizopo kwenye korodani kufa na kupelekea kuondolewa kwa korodani kwa njia ya upasuaji. Naam habari ndo hiyo! 🙄
🚨🚨 Mwanaume unapoanza kusikia maumivu ya korodani yaliyoanza bila sababu (pengine ajali au ugonjwa mwingine) tafadhali wahi hospitali (hasa hospitali ya wilaya au rufaa) iliyopo karibu.
📌📌 Korodani zinaweza kuokolewa ikiwa upasuaji wa kutoa korodani nje na kuzikunjua utafanyika ndani ya masaa sita (6) tu baada ya maumivu kuanza. Naam masaa sita pekee! 🤏🤓 Hivyo hakuna muda wa kupoteza.

🙏🏽🙏🏽 Tafadhali wasaidie wengine kujua kuhusu tatizo hili hasa vijana ili tuokoe kizazi hiki maana wanaume skuiz wamekuwa wachache sana na wanazidi kupungua 🙌🏾 FANYA KU SHARE IWAFIKIE NA WENGINE WENGI.

HIJAMA NI NINI (cupping therapy)Watu wanauliza👉Tiba ya vikombe ni aina ya zamani ya dawa mbadala ambayo mtaalamu huweka ...
04/06/2023

HIJAMA NI NINI (cupping therapy)

Watu wanauliza
👉Tiba ya vikombe ni aina ya zamani ya dawa mbadala ambayo mtaalamu huweka kikombe maalum kwenye ngozi yako kwa dakika chache ili kuunda kunyonya.

👉Watu huipata kwa madhumuni mengi, ikiwani pamoja na kusaidia kwa maumivu, kuvimba, mtiririko wa damu, utulivu na ustawi, na k**a aina ya massage ya tishu za kina.

👉Cupping hufanya nini hasa?
vikombe huongeza mzunguko wa damu kwenye eneo ambalo vikombe vimewekwa. Hi inaweza kupunguza mvutano wa misuli, ambayo inaweza kuboresha mtiririko wa damu kwa ujumla na kukuza ukarabati wa seli. Inaweza pia kusaidia kuunda tishu mpya zinazounganishwa na kuunda mishipa mpya ya damu kwenye tishu.

👉MAGONJWA SUGU YANAYOWEZA KUTIBIWA KWA KUTUMIA HIJAMA {Cupping therapy}
• Maumivu / majeraha ya jumla
• maumivu ya kichwa na kipandauso(migraine) • cholesterol nyingi (mafuta)
• ugonjwa wa arthritis na shida zingine za viungo au mfupa
Magonjwa ya kupumua k**a bronchiti sugu / kikohozi sugu/ sinusitis
• kifafa na shida ya neva
k**a kiharusi / kupooza / kufa ganzi
· kuvimbiwa /ugonjwa wa haja kubwa
• shida ya ngozi na (skin diseases)
• shida za hedhi na shida zingine za uke
• udhaifu wa kijinsia(nguvu za kiume)
X
• kukosa usingizi / wasiwasi na unyogovu
• mzunguko mbaya wa damu (circulate blood) •shinikizo la damu
• marundo ya damu (a blood clot) kumaliza hedhi (systm period)
• ugumba (infertility and problem ovaries) • kisukari (diabetec an diet plan) 2 week
* ukuaji wa nywele (hairgrowth)
• magonjwa ya moyo (heart diseases) • maumivu ya neva ya sciatica nk *tumbo kujaa gesi (gastritis ) •kiuno na magoti na mgongo mzima (uti) •matatizo ya miguu kuwaka moto na ganzi
tiba hii inatumiwa duniani kote na zaidi wachina na wahindi ndio tiba yao tegemezi nchini mwao jitahidi ufanye kwa kulinda afya yako kwa maradhi makubwa.

Ndgu Msomaji wa makala zetu K**a unahitaji huduma hii ya HIJAMA na upo katika wilaya ya CHATO please wasiliana na mtaalamu wa hijama yani Hijama Therapist Athuman Bagura AU

WHATSAPP:+255 757 746 852 ANAPATIKANA CHATO

Address

Kaengesa
Sumbawanga

Opening Hours

Monday 10:00 - 19:00
Tuesday 10:00 - 19:00
Wednesday 10:00 - 19:00
Thursday 10:00 - 19:00
Friday 10:00 - 19:00
Saturday 10:00 - 19:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when DR BWIRE Healthy Service posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to DR BWIRE Healthy Service:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram