27/08/2022
*KIWEMBE HERBAL PHARMAL*
*MWENDELEZO WA MAKALA NO1 HII NI NAMBA2
*TATIZO LA TUMBO KUJAA MAJI*
Kuna Aina Ngapi Za Ascites?
Kwa desturi, ascites hugawanywa katika aina kuu 2, transudative na exudative. Mgawanyo huu hutegemea kiwango cha protini kinachoonekana ndani ya maji hayo. Namna bora zaidi iliyotumika ni kutazama kiasi cha albumin kilichopo ndani ya maji (ascitic fluid) kikilinganishwa na kiasi kilichopo ndani ya albumin iliyopatikana ndani ya damu. Hii huitwa Serum Ascites Albumin Gradient au SAAG. Acites iliyotokana na pressure kwenye mishipa mikubwa ya damu ya ini (portal hypertension) huwa juu ya 1.1, na ascites kwa sababu nyingine huwa chini ya 1.1.
Tiba Ya Ugonjwa Wa Maji Kujaa Tumboni
Tiba ya ugonjwa wa maji kujaa tumboni kwa kiasi kikubwa itategemea chanzo halisi cha ugonjwa huu. Kwa mfano, peritoneal carcinomatosis au malignant ascites itatibiwa kwa kufanya upasuaji kuondoa eneo lililoathirika na saratani au kwa chemotherapy, wakati ascites iliyotokana na matatizo ya moyo itadhibitiwa kwa dawa za kutibu chanzo cha moyo kushindwa kufanya kazi vizuri au masharti katika kula.
Endapo maji kujaa tumboni kumetokana na uharibifu wa ini (cirrhosis), mgonjwa atasaidiwa kwa kushauriwa kupunguza matumizi ya chumvi na kumeza vidonge vya kutoa maji yaliyozidi mwilini. Vidonge hivyo vitamfanya atoe haja ndogo mara nyingi zaidi huku vikizuia utunzwaji wa maji mwilini. Pamoja na kuwa hii ni njia bora, aina nyingine za ugonjwa huu hazisikii tiba hii.
Hali ikiwa mbaya sana, operesheni ya kubadilisha ini inaweza kuwa ndiyo uamuzi wa mwisho. Tiba nyingine ni k**a zifuatazo:
Paracentesis
K**a tiba nyingine hazikutoa msaada mkubwa au k**a maji ni mengi sana, paracentesis hutumika. Hii ni njia ambapo daktari huingiza sindano tumboni na kutoa maji yaliyozidi nje ya mwili.
Lengo ni kupunguza msukumo ndani ya tumbo, na kumfanya mgonjwa ajisikie vizuri. Maji yanayotolewa yanaweza kufika lita 5, ingawa kuna wagonjwa wenye hali mbaya zaidi ambao hutolewa maji zaidi ya lita 10.
Shunts
Endapo maji yamejaa tumboni kutokana na kansa, madaktari wanaweza kutumia mpira kuondoa maji kutoka kwenye tumbo na kuyaingiza kwenye mtiririko wa damu.
Daktari huchoma sindano kwenye neva ya shingoni na kuweka shunt kupitia
kifuani. Shunt hiyo huunganisha uwazi wa tumbo na shingo, na kuingia kwenye veni. Na hivyo maji hutiririka kupitia mrija huo hadi kwenye mzunguko wa damu.
Chemotherapy
Chemotherapy inaweza kutumika kudhibiti saratani. Inaweza kufanywa kutumia mpira unaoingizwa tumboni, ingawa hakuna ushahidi wa kuwa njia hii ina matokeo bora.
Swali lakujiuliza jee???kuna dawa za mimea tiba zenye kutibu ugonjwa jawabu lake ndio ziko iko mimea ambayo mgonjwa hupewa anywe lengo atoe maji hayo kwa njia ya mkojo hadi maji yatakapo kwisha tumboni nahii ndio njia sahihi isiyo na madhara kwa mgonjwa nandio njia yakuondoa maji tumboni kwa haraka sana biidhini llahi.
*KIWEMBE HERBAL PHARMACY*
tunatoa huduma za dawa asili za mimea tiba pamoja nakuwashauri kuwaelimisha wenye magonjwa mbali mbali tupigie sasa.
โ๏ธ๐โ๏ธ+255652175774/+255787941413 tabibu.m.b.mwarizo.from.tanga.tanzania๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ๐น๐ฟ