09/07/2025
*Hizi ni dalili tano za ngiri (hernia) kwa mwanaume ambazo hujitokeza mara nyingi*
1️⃣ Uvimbishaji au uvimbe sehemu ya chini ya tumbo au kinena
Uvimbe huu huonekana zaidi wakati wa kusimama, kukohoa au kubeba vitu vizito. Mara nyingi hutokea upande mmoja wa kinena.
2️⃣ Maumivu au hisia ya kuchoma sehemu ya kinena
Mwanaume huhisi maumivu au kuchomachoma katika eneo la kinena, hasa anapoinama au kunyanyua vitu.
3️⃣ Maumivu yanayosambaa hadi kwenye korodani
Ngiri ya kinena inaweza kusababisha maumivu yanayoelekea moja kwa moja hadi kwenye korodani.
4️⃣ Hisia ya uzito au kushuka kwa kitu tumboni
Mwanaume huhisi kana kwamba kuna kitu kinavuta au kushuka ndani ya tumbo kuelekea kwenye kinena au korodani.
5️⃣ Maumivu huongezeka ukifanya shughuli ngumu
K**a vile kubeba mizigo, kufanya mazoezi au kukohoa – maumivu au uvimbe huongezeka.
🔴 Tahadhari:
Ngiri ikiachwa bila kutibiwa inaweza kuwa hatari kwa maisha, hasa ikiwa inasababisha kuharibika kwa sehemu ya utumbo. Ni vyema kumwona daktari kwa uchunguzi sahihi.