01/03/2025
☪️أسهل طريقة لختم القرآن الكريم في رمضان المبارك
☪️NJIA NYEPESI ZAIDI ZA KUKHITIMISHA (KUMALIZA) QUR AAN TUKUFU (MARA MOJA AU ZAIDI YA MARA MOJA) NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI WENYE BARAKA
طريقة ختم القرآن في خلال (30 يوم) كل يوم جزء من القرآن.
☪️Njia ya kwanza ya kumaliza Qur aan ndani ya siku thelathini (30) kila siku utasoma juzuu moja ktk Qur aan.
- الفجر : 4 صفحات
Swala ya alfajiri utasoma kurasa 4.
- الظهر : 4 صفحات
Swala ya adhuhuri utasoma kurasa 4.
- العصر : 4 صفحات
Swala ya alasiri utasoma kurasa 4.
- المغرب : 4 صفحات
Swala ya magharibi utasoma kurasa 4.
- العشاء : 4 صفحات
Swala ya ishaa utasoma kurasa 4.
طريقة ختم القرآن في (15 يوم) كل يوم خلال جزئين من القرآن.
🔹Njia ya pili ya kumaliza Qur aan ndani ya siku kumi na tano (15) kila siku utasoma juzuu mbili ktk Qur aan.
- الفجر : 8 صفحات
Swala ya alfajiri utasoma kurasa 8.
- الظهر : 8 صفحات
Swala ya adhuhuri utasoma kurasa 8.
- العصر : 8 صفحات
Swala ya alasiri utasoma kurasa 8.
- المغرب :8 صفحات
Swala ya magharibi utasoma kurasa 8.
- العشاء : 8 صفحات
Swala ya ishaa utasoma kurasa 8.
طريقة ختم القرآن في خلال (12 يوم) كل يوم جزئين ونصف من القرآن.
🔸Njia ya tatu ya kumaliza Qur aan ndani ya siku kumi na mbili (12) kila siku utasoma juzuu mbili na nusu ktk Qur aan.
- الفجر : 10 صفحات
Swala ya alfajiri utasoma kurasa 10.
- الظهر : 10 صفحات
Swala ya adhuhuri utasoma kurasa 10.
- العصر : 10 صفحات
Swala ya alasiri utasoma kurasa 10.
- المغرب : 10 صفحات
Swala ya magharibi utasoma kurasa 10.
- العشاء : 10 صفحات
Swala ya ishaa utasoma kurasa 10.
طريقة ختم القرآن في خلال ( 10 أيام ) كل يوم ثلاثة أجزاء من القرآن.
🔹Njia ya nne ya kumaliza Qur aan ndani ya siku kumi (10) kila siku utasoma juzuu tatu ktk Qur aan.
- الفجر : 12 صفحة
Swala ya alfajiri utasoma kurasa 12.
- الظهر : 12 صفحة
Swala ya adhuhuri utasoma kurasa 12.
- العصر : 12 صفحة
Swala ya alasiri utasoma kurasa 12.
- المغرب : 12 صفحة
Swala ya magharibi utasoma kurasa 12.
- العشاء : 12 صفحة
Swala ya ishaa utasoma kurasa 12.
هذا البرنامج لأصحاب الهمم العالية طريق ختم القرآن في خلال (6 أيام) كل يوم خمسة أجزاء من القرآن.
🔸Mpangilio huu na utaratibu huu na ratiba hii ni kwaajili ya watu wenye bidii na pupa mno na maazimio ya hali ya juu kabisa.
🔹Njia ya tano ya kumaliza Qur aan ndani ya siku sita (6) kila siku utasoma juzuu tano ktk Qur aan.
- الفجر : 20 صفحة
Swala ya alfajiri utasoma kurasa 20.
- الظهر : 20 صفحة
Swala ya adhuhuri utasoma kurasa 20.
- العصر : 20 صفحة
Swala ya alasiri utasoma kurasa 20.
- المغرب : 20 صفحة
Swala ya magharibi utasoma kurasa 20.
- العشاء : 20 صفحة
swala ya ishaa utasoma kurasa 20.
👈🏾انشرها في المجموعات فإنك فلا تدري كم من الأجر سيصلك حين يختم أحدهم القرآن الكريم بسببك.
👉🏾Sambaza na tawanya na eneza ujumbe huu ktk magrupu mbalimbali ya dini ya Uislamu au magrupu mbalimbali ya Waislamu, basi hakika yako wewe haujui utapata malipo kiasi gani wakati atakapomaliza mmoja wao Qur aan Tukufu (miongoni mwa watu watakaopata ujumbe huu) kwasababu yako.
🔺NYONGEZA KUTOKA KWA ALIYETAFSIRI:
🔸Ewe ndugu yangu Muislamu Mtukufu ALLAH akubariki na akuhifadhi, jitahidi sana kusoma Qur aan Tukufu ndani ya mwezi wa Ramadhani na usiwe mvivu, na chagua njia moja ktk njia hizo unayoweza uitumie au jiwekee utaratibu mwengine unaoweza uutumie na usijizuilie kheri,na hakika Qur aan Tukufu iliteremshwa ndani ya mwezi wa Ramadhani na haitokuwa jambo la sawa na si katika ukamilifu wa imani kuacha kuisoma Qur aan.
👈🏾قَالَ اللَّهُ تَعَالَى:
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ فَمَنْ شَهِدَ مِنْكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَنْ كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
👉🏾Amesema ALLAH Aliyejuu Mtukufu Ametukuka:
Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur aani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hesabu katika siku nyengine.ALLAH anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hesabu, na mumtukuze ALLAH kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.
Sura ya 2 aya ya 185.
🔹Ewe ndugu yangu Muislamu Mtukufu, jitahidi sana kujifundisha Qur aan Tukufu na wafundishe watoto wako Qur aan Tukufu, na chukulia umuhimu mkubwa sana swala la kujifundisha kitabu chako kitukufu, na chukulia umuhimu mkubwa sana wa kuwafundisha watoto wako kitabu chao kitukufu kuliko unavyochukulia umuhimu wa kuwatafutia rizqi, na ikiwa haukujifundisha Qur aan Tukufu, hautoweza kumaliza Qur aan Tukufu kwa kusoma vizuri zaidi.
🌟Tanbiih: Hakuna idadi maalum ya siku za kumaliza Qur aan bali, ni bora zaidi Muislamu ajitahidi kusoma Qur aan mara kwa mara, na asimalize Qur aan chini ya siku tatu, na ikiwa Muislamu anapupa mno na bidii zaidi na maazimio ya juu kabisa na akamaliza Qur aan chini ya siku tatu yaani akamaliza Qur aan kwa siku mbili au moja siyo haramu na wako baadhi ya waja wema waliofanya hivyo.
Lakini siku tatu ni bora zaidi..