21/04/2026
“Eucalyptus” —ndilo jina lake kisayansi, maarufu k**a Mkaratusi, ni miongoni mwa miti maarufu sana katika tiba asili kutokana na mafuta na majani yake kuwa na viambato vyenye nguvu za kiafya.
Matumizi ya Eucalyptus Katika Tiba za Jadi
1. Matatizo ya njia ya hewa
- Kutibu kikohozi, mafua, na sinusitis: Maji ya majani ya eucalyptus huchomwa kwenye moto, kisha mvuke huvutwa.
- Pumu (Asthma): Husaidia kupanua njia za hewa kwa kuvuta harufu ya mafuta au mvuke wa majani.
2. Maambukizi ya bakteria na fangasi
- Eucalyptus ina antibacterial na antifungal properties – hutumika kutibu vidonda, majipu, au upele wa ngozi kwa kupaka mafuta ya eucalyptus.
3. Maumivu ya misuli na viungo
- Mafuta ya eucalyptus hupakwa sehemu zenye maumivu k**a arthritis, baridi yabisi, na maumivu ya misuli ili kupunguza uvimbe na maumivu.
4. Homa na malaria
- Majani ya eucalyptus huchochea jasho na hivyo kusaidia kushusha homa. Pia hutumika kuondoa mbu wanaosababisha malaria.
5. Harufu mbaya ya mdomo
- Majani au mafuta yake hutumika k**a mouthwash ya asili, yanaua bakteria wa kinywani.
6. Kuondoa wadudu
- Mafuta ya eucalyptus huondoa kupe, chawa, na mbu – yanatumika k**a dawa ya kupaka au kunyunyiza.
7. Matatizo ya ngozi
- Hutumika kutibu chunusi, vidonda na upele kwa kupaka maji au mafuta ya eucalyptus.
Jinsi ya kutumia:
- Mvuke: Chemsha majani, jifukize na mvuke kwa dakika 5–10.
- Mafuta: Pakaa kwenye sehemu yenye maumivu au upele.
- Maji ya kuoga: Chemsha majani, changanya kwenye maji ya kuoga kwa kusafisha ngozi na kutuliza mwili.
Mdharau asili hufa kikatili