12/04/2026
🟢 Uzinduzi wa Tanga City Cup 2026 – Kuunganisha Michezo na Afya ya Jamii
Jana, 11 Aprili 2026, kulifanyika uzinduzi wa mashindano ya Tanga City Cup, yanayosimamiwa na Michezo Plus chini ya programu ya TangaYetu. Uzinduzi huo uliambatana na mchezo wa ufunguzi kati ya Majengo na Mwanzange, ukiwa ni ishara ya kuhamasisha mshikamano na maendeleo kupitia michezo.
Katika tukio hilo, waelimishaji wa Gift of Hope Foundation (GOHF) kupitia mradi wa Focus on Youth, Not the Substance ilishiriki kikamilifu kwa kutoa elimu ya uhamasishaji kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda afya na mustakabali wa vijana.
Ushiriki huu unaonesha namna michezo inavyoweza kuwa jukwaa muhimu la kufikisha ujumbe chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla, na kuchangia katika kujenga kizazi chenye afya na maamuzi sahihi.
.
ISSUP TANZANIA
# Coastal Union