Yuma macronutrients

Yuma macronutrients Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Yuma macronutrients, Medical and health, Tanga.

Nawasaidia wanaume&wanawake kuboresha afya zao kwa ushauri wa afya, lishe na program salama zinazounga mkono mwili kama vile;
✅Kisukari(diabetes)
✅Shida za uzazi (wanawake&wanaume)
✅Maumivuya mgongo,miguu na mikono,ganzi n.k karibu sana.

17/04/2026

JE, UNAFAHAMU KUHUSU OVARIAN CYST, AINA ZAKE, SABABU, DALILI NA MADHARA YAKE.......?

🌸 Maana ya Ovarian cyst
_Ovarian cyst ni mfuko uliojaa maji au damu unaotokea kwenye ovari (mfuko wa mayai ya mwanamke). Mara nyingi uvimbe huu unaweza kuwa mdogo na huondoka wenyewe, lakini wakati mwingine hukua na kusababisha matatizo.

🧬 Aina 2 kuu za ovarian cyst
1. Functional cyst (uvimbe wa kawaida wa mzunguko wa hedhi)
_Hutokea wakati wa mchakato wa kawaida wa ovulation
_Ni wa muda mfupi na mara nyingi hupotea wenyewe
Aina zake:
_Follicular cyst
_Corpus luteum cyst

2. Pathological cyst (uvimbe usio wa kawaida)
_Hutokana na matatizo ya seli au tishu za ovari
_Huweza kuwa mkubwa na kudumu muda mrefu
Mfano:
_Dermoid cyst
_Endometrioma (husababishwa na endometriosis)

⚠️ Sababu za ovarian cyst
_Mabadiliko ya homoni (hormonal imbalance)
_Ovulation isiyo ya kawaida
_Endometriosis
_Ujauzito (kwa baadhi ya aina)
_Maambukizi ya fupanyonga (PID)
_Historia ya familia

⚠️ Dalili za ovarian cyst
Wengi hawana dalili, lakini ikiongezeka inaweza kusababisha:
_Maumivu ya chini ya tumbo (upande mmoja)
_Tumbo kujaa au kuvimba
_Maumivu wakati wa tendo la ndoa
_Hedhi isiyo ya kawaida
_Kukojoa mara kwa mara (k**a cyst ni kubwa)
_Maumivu ya ghafla makali (ikipasuka)

🧨 Madhara (ikiachwa bila matibabu)
_Kupasuka kwa cyst (rupture) → maumivu makali na damu ndani
_Kugeuka kwa ovari (ovarian torsion) → kukata mzunguko wa damu
_Ugumba (infertility) kwa baadhi ya aina
_Maumivu ya muda mrefu ya nyonga
_Kuvimba kwa tumbo
_Hatari ya maambukizi au saratani (kwa aina chache sana).
🇺🇸

17/04/2026

🔥 DALILI ZA AWALI ZA SARATANI YA TEZI DUME 🔥
Usipuuzie ishara ndogo ndogo za mwili wako! Saratani ya tezi dume huanza taratibu bila maumivu makali mwanzoni.

⚠️ Zifahamu dalili hizi mapema:
• Kukojoa mara kwa mara
• Mkojo kukatika katika mtiririko
• Damu kwenye mkojo au shahawa
• Maumivu wakati wa kumwaga

• Maumivu mgongoni, nyonga au hips
💡 Uchunguzi wa mapema unaweza kuokoa maisha!.

14/04/2026

🦵 MAGOTI NA VIUNGO KUSAGIKA: JUA MAPEMA, CHUKUA HATUA!

🔎 Sababu za kusagika kwa magoti na viungo
_Uzee (uchakavu wa cartilage ya viungo)
_Uzito kupita kiasi (shinikizo kubwa kwenye magoti)
_Majeraha ya viungo (kuanguka au michezo)
_Kazi nzito au kusimama muda mrefu
_Magonjwa ya mifupa (k**a arthritis)

⚠️ Dalili zake
_Maumivu ya mara kwa mara kwenye magoti au viungo
_Kukak**aa (hasa asubuhi)
_Kuvimba na joto kwenye kiungo
_Kusikia mlio wa kusaga (cracking sound)
_Kupungua uwezo wa kusogeza kiungo

🚨 Madhara yake
_Uharibifu wa kudumu wa viungo
_Kushindwa kutembea au kufanya kazi vizuri
_Ulemavu wa muda mrefu
_Maumivu sugu yanayoathiri maisha ya kila siku

💡 Ushauri:
Usisubiri hali iwe mbaya! Pata ushauri wa kitaalamu mapema ili kulinda afya ya viungo vyako.

12/04/2026

💖 Zifahamu Awamu Zako, Itawale Hedhi Yako! 🌸
Kipindi cha hedhi sio "siku za maumivu" tu. Ni mzunguko mzima wa mabadiliko ya kimaumbile na kihisia yaliyo na hatua nne tofauti.
Mzunguko wako unaweza kuathiri:
✅ Kiwango chako cha nishati na uchovu.
✅ Mood na hisia zako.
✅ Matamanio yako ya chakula na uzito.
✅ Hali yako ya ngozi na nywele.
👉 👉 Angalia slide zetu zilizofasiriwa Kiswahili ili kujua hasa nini cha kutarajia katika kila awamu:
1️⃣ Awamu ya Hedhi (Days 1-5) 🛑
2️⃣ Awamu ya Folikula (Days 6-14) 🌿
3️⃣ Awamu ya Ovulesheni (Day 15) ✨
4️⃣ Awamu ya Luteali (Days 16-28) 🌙
Elimu hii ni ufunguo wa kujitunza vizuri, kupanga mambo yako, na kuishi kwa furaha kila siku ya mwezi. Share post hii kwa marafiki zako ili sote tuelimike! 🔄

.

11/04/2026

*JE WEWE NI MWANAMKE NA UNAPATWA NA HALI HII?*

KUTOKWA NA UCHAFU UKENI PAMOJA NA MIWASHO

Mwanamke, Je umewahi kuhisi miwasho ukeni mpaka unakosa amani kwabkujikuna mpaka vidonda .miwasho ikifuatana na uchafu mweupe mzito k**a maziwa ya mgando? Usijifiche! Hii ni ishara ya tatizo linalohitaji kuangaliwa kwa makini.

*🔬 CHANZO KIKUU:*
Hali hii mara nyingi husababishwa na maambukizi ya fangasi ukeni, hasa aina inayoitwa Candida albicans.

*🔎 DALILI ZA KUWA NA FANGASI WA AINA HII UKENI:*

UTAKUMBWA NA HALI HIZI

✅ Miwasho mkali au ya wastani ukeni
✅ Uchafu mweupe mzito k**a maziwa ya mgando
✅ Harufu ya kawaida au kutokuwepo kabisa kwa harufu
✅ Maumivu wakati wa kukojoa au kushiriki tendo la ndoa
✅ Ngozi ya uke kuwa nyekundu na kuvimba

*⚠️ FANGASI* *HAZISABABISHWI NA UCHAFU!*
Hata mwanamke msafi sana anaweza kuzipata kutokana na:
➖ Matumizi ya antibiotics
➖ Mabadiliko ya homoni (mimba, hedhi n.k.)
➖ Kuvaa nguo za ndani zisizopitisha hewa
➖ Kisukari kisichodhibitiwa
➖ Msongo wa mawazo au kinga ya mwili kushuka

*🧼 JE, UNAJITIBUJE?*
❌ Usitumie sabuni kali au dawa za kujichua bila ushauri
✅ Tumia tiba ya kitaalamu au ya asili ya kuua fangasi inayoiywa FEMININE CLEANSER
✅ Va nguo za pamba PEDI ya pamba.

10/04/2026

GANZI SIYO KAWAIDA – NI ISHARA YA UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO MWILINI
Kwanini unapata ganzi?
Ganzi hutokea pale mishipa ya fahamu inapokosa virutubisho muhimu au inapobanwa, hivyo ujumbe wa fahamu kushindwa kupita vizuri.

DALILI 4 ZA GANZI:
1️⃣ Kufa ganzi mikono au miguu
2️⃣ Kuwashwa au kuhisi sindano sindano
3️⃣ Kukosa nguvu kwenye viungo
4️⃣ Kupoteza hisia ya joto au baridi

SABABU 4 KUU:
1️⃣ Upungufu wa vitamini B (hasa B1, B6, B12)
2️⃣ Kisukari (sukari kuharibu mishipa ya fahamu)
3️⃣ Mzunguko duni wa damu
4️⃣ Kubanwa kwa mishipa (mf. kukaa muda mrefu vibaya)

MADHARA 3 IKIACHWA BILA TIBA:
⚠️ Kudhoofika kwa mishipa ya fahamu
⚠️ Kupoteza nguvu na ufanisi wa viungo
⚠️ Hatari ya vidonda na maumivu sugu

Kwanini unapaswa kutumia SUPPLEMENTS?
✔️ Hurejesha virutubisho muhimu haraka
✔️ Hulinda na kutengeneza mishipa ya fahamu
✔️ Huboresha mzunguko wa damu na nguvu ya mwili
✔️ Husaidia kuzuia madhara ya muda mrefu
👉 Linda afya yako mapema kabla ganzi haijageuka ugonjwa mkubwa.

10/04/2026

*SIFA ZA HEDHI BORA YA MWANAMKE*

Hedhi ni kipindi maalumu katika mzunguko wa siku za mwanamke mwenye umri wa kuzaa. Hedhi bora ni dalili ya afya njema ya uzazi. K**a wewe ni mwanamke na utaona kuna kitu hakipo sawa katika hedhi yako ni vema uwahi kupata msaada ili kuboresha afya yako ya uzazi.

● *Zifuatazo ni sifa za hedhi iliyobora:*

1. Hedhi ilibora hupatikana mara moja kwa mwezi yaani k**a mzunguko wako ni siku 28 basi hedhi yako itapatikana kila baada siku 28. K**a hedhi haitabiriki ujue kuna shida ambayo unapaswa kuitatua ili upate hedhi iliyobora.

2. Hedhi iliyobora haiambatani na maumivu makali, kwa kawaida maumivu ya hedhi hayapaswi kumfanya mwanamke kuacha kufanya shughuli zake za kawaida. K**a unapata maumivu makali sana wakati wa hedhi kiasi cha kushindwa kufanya kazi zako za kawaida basi ujue hedhi yako ina shida.

3. Hedhi iliyobora hupatikana siku tatu mpaka saba. Katika mzunguko wa mwezi siku za hedhi zinapaswa kuwa tatu mpka saba. Chini au zaidi ya hapo ni ishara ya hatari katika afya yako ya uzazi.

4. Hedhi iliyobora damu yake si nzito sana yenye mabonge mabonge au nyepesi sana k**a maji yenye rangi ya damu. K**a unaona unapata hedhi nzito sana au nyepesi sana ni vema uwahi kupata matibabu.

5. Kiwango cha damu ya hedhi iliyobora huwa ni cha kawaida si damu nyingi sana inayopelekea mwanamke kubadili (pedi) mara nyingi kwa siku, au damu chache sana vitone tu vichache vya damu kila mwezi.

MATATIZO YA HEDHI MFANO

1. Kutoona hedhi kabisa
2. Kupata hedhi yenye maumivu
3. Kupata hedhi yenye mabonge ya damu k**a punje za mahindi
4. Hedhi kutoka zaidi ya muda wa kawaida mfano zaidi ya siku saba na zaidi
5. Kuingia hedhi mara mbili kwa mwezi
HII NI CHANGAMOTO YA MVURUGIKO WA HOMONI

naweza kukusaidia ukapona ndani ya siku 30 tu nipigie moja kwa moja kupitia namba hii ya ofisi.

09/04/2026

🚨 HATARI! KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA UJAUZITO SI JAMBO LA KUPUUZIA 🚨

🤰 Je, umewahi kuona damu ukiwa mjamzito?Hii inaweza kuwa ishara ya tatizo linalohitaji uangalizi wa haraka!

⚠️ SABABU ZAKE:

🔴 Kujishikiza kwa mimba (Implantation – mwanzo wa ujauzito)🔴 Maambukizi kwenye uke au mlango wa kizazi🔴 Mimba kutoka (Miscarriage)🔴 Mimba nje ya mfuko wa uzazi (Ectopic pregnancy)🔴 Tatizo la placenta (Placenta previa au abruption)

🚫 MADHARA YAKE:

❗ Kupoteza ujauzito❗ Hatari kwa maisha ya mama❗ Upungufu wa damu (Anemia)❗ Mtoto kuzaliwa kabla ya muda

💡 USHAURI MUHIMU:

✅ Usikae kimya – nenda hospitali mara moja✅ Pumzika na epuka kazi nzito✅ Fuatilia dalili nyingine k**a maumivu makali

📲 Afya yako ni muhimu!

Anemia UzaziSalama TanzaniaHealth JaliMaisha

08/04/2026

🩸 Je, Hedhi Yako Inakuambia Nini Leo? 🩸
Rangi ya damu ya hedhi ni zaidi ya mabadiliko ya kawaida ya mwili—ni lugha ambayo mwili wako unatumia kuwasiliana nawe kuhusu afya ya homoni zako na mfumo wako wa uzazi kwa ujumla. 🌸✨

Kuelewa rangi hizi kutakusaidia kujua nini ni cha kawaida na wakati gani unapaswa kuchukua hatua. Hebu tuziangalie:

1️⃣ Rangi ya Pinki (Light Pink): Huashiria mtiririko mwepesi au kiwango kidogo cha kichocheo cha estrogen.
2️⃣ Nyekundu Inayong'aa (Bright Red): Hii ni damu safi na yenye afya, mara nyingi huonekana wakati wa siku za katikati za mzunguko.
3️⃣ Nyekundu Iliyoiva (Dark Red): Ni damu ya zamani kidogo, mara nyingi huonekana mwanzoni au mwishoni mwa hedhi.
4️⃣ Rangi ya Chungwa (Orange): Inaweza kuwa ishara ya maambukizi (Infection) au mchanganyiko wa majimaji ya mlango wa uzazi. Kuwa mwangalifu!
5️⃣ Rangi ya Kijivu (Gray): Hii ni ishara kubwa ya maambukizi. Ukiona hivi, tafadhali nenda hospitali kupata ushauri wa daktari.
6️⃣ Rangi ya Udongo/Kahawia (Dark Brown): Hii ni damu iliyokaa muda.

06/04/2026

*JE, KISUKARI KINAWEZA KUATHIRI NGUVU ZA KIUME AU HAMU YA TENDO LA NDOA?*
✔️Ndiyo kisukari kinaweza kuathiri nguvu za kiume na pia kupunguza hamu ya tendo la ndoa, hasa k**a hakijadhibitiwa vizuri.
▪️Hii hutokea kwa sababu:
• sukari ya juu huathiri mishipa ya fahamu (neva)
• hupunguza mzunguko wa damu kwenye viungo vya uzazi
• na huweza kuathiri homoni pamoja na hali ya kisaikolojia
▪️Matokeo yake yanaweza kuwa:
• kupungua kwa nguvu za kiume (erectile dysfunction)
• kushuka kwa hamu ya tendo la ndoa
• au kushindwa kuridhika kikamilifu
Kwa baadhi ya watu, dalili hizi huanza taratibu bila kutambulika mapema.
👉 Muhimu: Kudhibiti sukari ya damu, lishe bora, na ufuatiliaji wa afya kwa karibu husaidia kulinda uwezo wa mwili kufanya kazi kawaida.
📌Afya ya uzazi ni sehemu ya afya kwa ujumla na inahitaji uangalizi k**a zilivyo sehemu nyingine za mwili.

06/04/2026

⚫Changamoto za mifupa, maungio na misuli ni miongoni mwa matatizo yanayoathiri watu wengi katika maisha ya kila siku, hasa kutokana na mtindo wa maisha usio na harakati za kutosha, lishe duni, kuzeeka, au kazi zinazohusisha kukaa au kusimama muda mrefu.
✔️Changamoto hizi hazipaswi kupewa nafasi iwapo mwili unapata msaada sahihi wa lishe matumizi ya virutubisho bora pamoja na lishe kamili yanaweza kusaidia:
•Kuimarisha mifupa kwa kuongeza madini k**a Calcium na Vitamin D
•Kupunguza uvimbe kwenye maungio kwa kutumia virutubisho k**a Omega-3 na antioxidants
•Kusaidia urejeshaji wa cartilage kwa virutubisho k**a Glucosamine na Chondroitin
•Kuimarisha misuli na kupunguza maumivu kupitia Protein na Magnesium.
📌Kwa kuzingatia lishe bora, matumizi sahihi ya virutubisho, pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara, inawezekana kupunguza kwa kiwango kikubwa au hata kuzuia kabisa matatizo ya mifupa, maungio na misuli mwili wenye afya huanza na msingi mzuri wa lishe hivyo chagua kula kwa uangalifu ili kuishi bila maumivu.

Address

Tanga
211XX

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Yuma macronutrients posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share