Health centertz

  • Home
  • Health centertz

Health centertz ELIMU USHAULI TIBA za MAGONJWA MBALI MBALI
�AFYA YA UZAZI
�MAGONJWA YA WANAUME
�MAGONJWA YA WANAWAKE
�KISUKARI,PRESHA NA MISULI
�MATATIZO YOTE SUGU

27/04/2023

Watu wengi wanasumbuliwa na haya matatizo usijihisi mnyonge na kykata tamaa msaada upo njoo tukusaidie urudishe furaha Yako

Tupo Dar es salaam mwenge TGB
Tupigie 0753121728

Like
Follow us .
🇹🇿

🛑 *UJUE UGONJWA WA P.I.D*Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa k...
25/04/2023

🛑 *UJUE UGONJWA WA P.I.D*

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana k**a cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu k**a salpingitis.

*_PID husababishwa na nini?_*

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.

*Je mwanamke huambukizwaje PID?*

Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na

✅Kufanya ngono isiyo salama.

✅Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)

✅Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)

✅Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) k**a njia mojawapo ya uzazi wa mpango.

✅Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.

*Dalili za PID ni zipi?*

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni :-

✅Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu

✅Kupata maumivu ya mgongo.

✅Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.

✅Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.

✅Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

✅Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi.

✅Kupata homa.

✅Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
Pia kutapika.

⏩Ugonjwa huu wa Pelvic Inflammatory Diseases *P.I.D* unakuwa kwa Kasi kubwa na baadhi ya wanawake hupata madhara makubwa baadae hususani Ugumba kutokana na kupuuzia matibabu. Ikiwa unaona dalili tajwa hapo juu jitahidi kuanza matibabu taratibu kabla haujapata madhara ambayo yanaweza kugharimu Maisha yako kwa ujumla.
✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿✍🏿
*JIKINGE NA P.I.D epuka UGUMBA*
wasiliaana nasi tutakusaidia Kwa tiba iliyo sahihi na uhakika

0653121727

🇹🇿

YES WE ARE PROFESSIONAL 👍👍Contact+255 653 121 728+255 757 174 859LikeFollow us .           🇹🇿               #           ...
25/04/2023

YES WE ARE PROFESSIONAL 👍👍




Contact
+255 653 121 728
+255 757 174 859

Like
Follow us .
🇹🇿 #

TATIZO LA KUPATA HEDHI NYINGI KUPITA KIASI ( HEAVY ME**ES )Kupata hedhi kupita kiasi ni moja ya matatizo ya uzazi yanayo...
25/04/2023

TATIZO LA KUPATA HEDHI NYINGI KUPITA KIASI ( HEAVY ME**ES )

Kupata hedhi kupita kiasi ni moja ya matatizo ya uzazi yanayosumbua wanawake wengi.

•Je ni wakati gani mwanamke anatakiwa kuhisi kuwa anapata hedhi kupita kiasi?

👉Unapata hedhi inayozidi siku 7.

👉Unapata hedhi nzito inayofanya ubadiri pedi moja ndani ya masaa mawili.

👉Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuvaa pedi zaidi ya moja.

👉Unapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje.

👉Unapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi.

👉Hedhi inayotoka na mabonge

•Sababu gani huweza kuchangia mwanamke kupata hedhi nzito kupita kiasi?

1.Vivimbe kwenye kuta za mji wa kizazi;

✍🏻vivimbe hivi sio saratani huitwa fibroids

2.Yai kupevuka bila mpangilio (Irregular ovulation) ;

✍🏻hali hii husababisha kuta za mji wa mimba zivimbe na kuwa nene hivyo kutoa damu nyingi. Hutokea zaidi kipindi cha kuvunja ungo na kipindi cha kukaribia ukomo wa hedhi.

3.Matatizo ya kugandisha damu

4.Matumizi ya dawa za kuzuia damu kuganda.

5.Baadhi ya wanawake waliotumia vitanzi (IUD) hasa ndani ya mwaka wa kwanza.

6.Maambukizi ya mji wa mimba na mirija ya uzazi (PID).

7.Endometriosis

8.Saratani ya mji wa kizazi;

✍🏻kwa kinamama waliofikia umri wa ukomo wa hedhi. Wakianza kupata hedhi isiyokoma huweza kuwa dalili ya ya saratani ya mji wa kizazi

ATHARI ZA HEDHI NZITO KUPITA KIASI KWENYE AFYA

1.Hedhi nzito kupita kiasi huchangia wanawake wengi kupata upungufu wa damu.

2.Hedhi kuwa nzito kupita kiasi huweza kuwa ni dalili ambao unahitaji tiba ya haraka.

3.Huweza kuchangia kudhoofisha afya ya akili ya mwanamke ikiwemo kujiamini na wasiwasi

Contact Us No:+255653121728

Like
Follow us .
🇹🇿

Dalili Za Upungufu Wa Mbegu Za Kiume Dalili kubwa ya kuwa na upungufu wa mbegu za kiume ni kukosa uwezo wa kumpa mimba m...
25/04/2023

Dalili Za Upungufu Wa Mbegu Za Kiume


Dalili kubwa ya kuwa na upungufu wa mbegu za kiume ni kukosa uwezo wa kumpa mimba mke. Kunaweza kutokea dalili nyingine za wazi. Dalili nyingine zinaweza kuwa:
Matatizo katika tendo la ndoa – kwa mfano, kukosa hamu ya tendo la ndoa au matatizo ya uume kusimama kwa muda mrefu ili kukamlisha tendo la ndoa.
Maumivu, uvimbe kwenye maeneo ya korodani
Kupungua kwa nywele za usoni au za mwilini au ishara nyingine za dosari za homoni.

Uonapo dalili hizi wasiliaana nasi tutakusaidia 0653121728

Like
Follow us .
🇹🇿

*SABABU ZINAZOPELEKEA MAUMIVU YA MGONGO.*♻️KUBEBA VITU VIZITO.Hii sababau ya kwanza ya maumivu ya mgongo hasahasa utokea...
25/04/2023

*SABABU ZINAZOPELEKEA MAUMIVU YA MGONGO.*

♻️KUBEBA VITU VIZITO.
Hii sababau ya kwanza ya maumivu ya mgongo hasahasa utokea pale mtu akianza kubeba vitu vizito katika umri mdogo na baadae pingili za mgongo huanza kuchoka na kugundulika kwamba anatatizo la uti wa mgongo.

♻️PINGILI KUISHIWA MAFUTA.
Katika mwili wa mwanadamu kuna pingili thelathini na tatu kila pingili ina kazi yake,pengine pingili huishiwa mafuta kwa sababu ya maambukizi au kwa sababu ya kutokula mlo kamili wa vyakula vya kuongezea mafuta mwilini hali hii usababisha mafuta mwili kuisha na pengine pingili usuguana hali hii upelekea maumivu makali kwenye uti wa mgongo kwa msuguano wa pingili.

♻️KUPATA AJALI.
Pengine maumivu ya mgongo yanasababishwa na kupata ajali na kuvunjika kwa baadhi ya pingili,hali hiii usababisha maumivu ya mgongo hata k**a mtu akitibiwa k**a kuna sehem ilibakia na jeraha kuna kipindi maumivu uumtokea hasa wakati wa baridi.

♻️UZITO WA MWILI KUWA MKUBWA.
Ukilinganisha na mifupa na nyama pengine maumivu ya mgongo yanasababishwa na kuongezeka kwa uzito wa mwili pale ambapo mifupa imeelemewa na uzito kwa hivyo maumivu ya mgongo uongezeka na kusababisha hali ya mtu kuwa mbaya.

♻️MIKAO YA MUDA MREFU.
Pengine maumivu ya mgongo yanasababishwa na kukaa muda mrefu sehem mmoja bila kushughulisha mwili wako.

*DALILI ZA MAUMIVU YA MGONGO.*
〽️Maumivu makali wakati wa kukaa

〽️Maumivu wakati wa kuinama.

〽️Maumivu wakati wa baridi.

〽️Maumivu makali wakati umesimama muda mrefu.

〽️Maumivu wakati wa kutembe kwa muda mrefu.

〽️Maumivu makali wakati wa kubeba vitu vizito nk.

KUPATA TIBA HII TUPIGIE
*0653121728*

Like
Follow us .
🇹🇿

Aina 15 ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume,na kuweka mwili sawa.1.Tende.Katika kila gram (100) ndani ya tende kuna ...
25/04/2023

Aina 15 ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume,na kuweka mwili sawa.

1.Tende.

Katika kila gram (100) ndani ya tende kuna virutubisho kwa asilimia k**a ifuatavyo.

Chuma (iron). 5.50ppm.

wanga (cabohydrate) 78.8%.

Nishati (energy) 317kcal.

Hamirojo (protin)2.5%.

Mafuta (fat).0.4%.

Kamba kamba (fiber)4%.

Madini 2.1%.

Unyevu nyevu (moisture)15.3%.

Fructose 27%.

Grucose (Sukari) 35%.

Faida nyingine za tende.

1.Huongeza damu ukichanganya na maziwa

2.Husaidia kuzalisha manii kwa wingi

3.Huongeza nguvu za kiume.

4.Huzidisha hamu ya tendo la ndoa.

2.Zabibu.

Huongeza sana nguvu za kiume,
wengi hupenda kuyaita "viagra"kwa sababu ya ufanyaji kazi mwilini. husaidia mzunguko wa damu,pia huondoa cholesterol

3.Chocolate.

Husaidia kuongeza stamina,kwa sababu ina viambato vya phenylethylamine na Alkaloid

Phenylethylamine.
hupelekea kujisikia vizuri.

Alkaloid.
Huongeza stamina wakati wa tendo la ndoa.

4.Ndizi.

Ni chanzo kikubwa cha vitamini B,ambacho ni muhimu katika tendo la ndoa,ina kimeng'enyo cha bromelan ambacho huongeza Ashk wakati wa tendo la ndoa.pia huongeza stamina.

5.Tangawizi.

Husisimua sana mzunguko wa damu.tangawizi imekuwa ikitumika sana katika maeneo ya Asia kwa ajili ya wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume.

6.Tunda la komamanga.

Ni aina ya matunda yenye rangi nyekundu na muonekeno k**a apple.husaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea uwezo na hamasa wakati wa tendo la ndoa na kupoke hisia kwa urahisi.

7.Mtini.

Ni matunda yenye kiwango kikubwa sana cha amino asid,ambayo ni kiungo kikubwa cha Kuzalisha homoni mwilini.

8.Karanga.

NI Chanzo kikubwa sana cha kurekebisha Protini mwilini,pia husaidia kuweka vizuri mzunguko wa damu,na kusaidia kuzalisha homoni ambayo ni muhimu kwa tendo la ndoa.

9.Asali.

Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu za kiume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kutibu uhanithi kutokana na uwezo wake k**a kiamshaji/chaji kwa wanandoa. Tumia vijiko 2 asubuhi na 2 jioni.

10.Kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu kina Allicin, kiambato kinachosaidia kuweka vizuri mzunguko wa damu.Pia Hupunguza tatizo la damu kuganda katika mishipa ya damu

11.Samaki aina ya pweza na chaza.

Hutoa madini aina ya zink ambayo huzalisha vichocheo vinavyoleta msisimko kwa wanandoa.

12.Ugali wa dona.

Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya na kuongeza nguvu za kiume.

Ongeza nguvu za kiume kwa kula ugali wa dona kila siku.

13.Maji.

Maji huchukua karibu asilimia (70%) katika mwili wa binadamu.

Ambapo;

Mifupa ina karibu asilimia (25%) ya maji.

Damu ina karibu asilimia(85%) ya maji.

NB.Damu ndio husababisha uume kusimama.

Misuli ya mwili ina karibu(75%) ya maji.

Ubongo una karibu asilimia(85%) ya maji.

Kunywa maji kila siku kabla ya kusikia kiu,Ikiwa mwili utakosa maji utajikopa maji toka katika ubongo,na wewe utapatwa na ‘kichwa kizito’ au kichwa kuuma ambacho kinaweza kupelekea maumivu ya kichwa.

unywaji wa maji kwa wingi hutusaidia kuweka sawa mzunguko wa damu pia huongeza akili na uwezo wa kufikili.

Kwa matumizi bora ya maji kunywa walau glass 8 kwa siku, na kunywa glass 1 ,kila unapoenda kulala.

14.Tikiti maji.

Lina vitamin A ambayo huondoa sumu mwilini,vitamini C huboresha kinga,hukinga uharibifu wa seli,husaida ubongo kufanya kazi vema,husafisha damu,na kukinga shinikizo la damu,

Hutibu nguvu za kiume ukila na mbegu zake.

15.Mbegu za maboga.

Huondoa msongo wa mawazo, Hutibu matatizo ya ngiri ,huondoa cholestrol,Zina madini ya zink ambayo ni muhimu kwa Mwanaume,zinaongeza wingi wa mbegu za kiume (s***m count), ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona kazi yake

Like
Follow us .
🇹🇿

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKEVidonda vya tumbo(Ulcers) ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi kutokana na mfu...
20/04/2023

FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE

Vidonda vya tumbo(Ulcers) ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi kutokana na mfumo wa Maisha, ulaji mbaya na Mazingira tunayoishi Kwa ujumla. Ugonjwa huu unasababisha kuwa na michubuko katika kuta za tumbo au utumbo mdogo na hivyo kusababisha maumivu makubwa ya tumbo.

Wakati mwingine vidonda hivi huonekana kati ya tumbo na utumbo mdogo hivyo kitaalam unaitwa PEPTIC ULCERS, aina hii ya vidonda vya tumbo huwaathiri sana Wanaume kuliko wanawake. Bacterium' Helicobacter Pylori ndio husababisha ugonjwa huu.

DALILI ZA KUWA NA VIDONDA VYA TUMBO

Mwili kuchoka bila sababu maalum
Kuumwa mgongo au kiuno
Kupungukiwa nguvu za kiume
Kizunguzungu
Kukosa Usingizi
Kichefuchefu
Kiungulia
Tumbo kujaa gesi
Tumbo kuwaka moto
Kukosa choo au kupata choo kwa shida
Kutapika nyongo
Kutapika damu au kuharisha
Sehemu za mwili kupata ganzi
Kukosa hamu ya kula
Kusahau sahau na hasira bila sababu
Hizo ni baadhi tu ya dalili za kuwa na vidonda vya tumbo lakini zipo nyingi, hivyo basi pindi uonapo moja kati ya hizo dalili ni vyema ukaenda kupima vidonda vya tumbo mapema.

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO
Tuna dawa nzuri sana ya kutibu vidonda vya tumbo hakika utapona kabisa. Dawa hii ina uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo hata k**a vimekuwa sugu Kwa miaka mingi vitapona tu.


Kwa mahitaji ya tiba hii tutafute

Piga 0653121728
🇹🇿

ZINGATIA HAYA;✅Usafi wa Uke kwa maji masafi ya kawaida.✅Epuka povu la sabuni kuingia ndani ya uke.✅Anza mbele kurudi nyu...
20/04/2023

ZINGATIA HAYA;

✅Usafi wa Uke kwa maji masafi ya kawaida.

✅Epuka povu la sabuni kuingia ndani ya uke.

✅Anza mbele kurudi nyuma wakati wakujisafisha mara baada ya kumaliza Haja kubwa/ndogo.

✅Unapohitaji kujikausha Uke wako tumia kitambaa safi na laini kabisa kuzuia michubuko.

✅Usitumie vitu vyenye kemikali/Tindikali au perfumes (manukato) ukeni. Mfano:- whipes

✅Unaweza kutumia Natural Cleanser, Cleanser/kisafisho maalumu (ASILIA kabisa) kwa Usafi salama na kinga ya Uke.

NB; Bacteria wanaoshambulia Kizazi hupitia UKENI TU,siyo puani, sikioni wala mdomoni, hivyo kujali mazingira ya Uke wako ni moja ya HATUA kubwa ya kuwa salama.

Karibu TUKUSAIDIE (USHAURI & TIBA)

Contact Us: +255653121728

Utungaji mimba hutokea kipindi yai la mwanamke linapokutana na seli za gamete za kiume zilizokomaa (manii).Inaweza chuku...
20/04/2023

Utungaji mimba hutokea kipindi yai la mwanamke linapokutana na seli za gamete za kiume zilizokomaa (manii).

Inaweza chukua dakika 45 mpaka masaa 12 kwa manii kufika katika mirija ya falopiani ambapo mimba hutungiwa. Hata hivyo, manii yanaweza kuendelea kuishi ndani ya mwili wa mwanamke mpaka siku saba, hivyobasi utungaji wa mimba unaweza kutokea siku yoyote katika wiki ifuatayo baada ya kujamiana, k**a upo katika siku za kutoa mayai(ovulation).

•Ndani ya mwili wa mwanamke: jinsi yai linavyotungwa
Kwa wanawake, uwezekano wa mimba unaanzia katika ovari zake.
Hizi ni ogani ndogo mbili zenye umbo la yai zilizoshikiliwa katika kila upande wa mjii wa mimba(uterasi).
Ovari zimejazwa mayai ambayo yalitengenezwa kabla ya kuzaliwa. Kila mtoto mchanga wa k**e anazaliwa na milioni 1 mpaka 2 ya mayai kwa kila ovari yake.

•Mayai mengi yanaanza kufa mapema na mengine kupungua taratibu kadiri unavyozidi kukua. Mara unapoanza hedhi, kawaia kati ya miaka 10 na 14, ni mayai 600,000(laki sita) tu yanaweza kuwepo.

•Katika umri wa miaka 30, wanasayansi wamekokotoa ni ttakribani mayai 72,000 yanaweza kubakia.
Kuna uwezekano wa kuzalisha mayai 400-500 katika kipindi cha miaka yako ya kuzaa, ambayo ni kati ya hedhi yako ya kwanza na wakati wa kukatika hedhi.

•Katika kila mzunguko wa hedhi,mara nyingine baada ya hedhi yako, kati ya mayai matatu na 30 yanaanza kukua katika kila moja ya ovari zako. Yai lililoiva linakua la kwanza kutolewa kupitia mfumo wa utoaji wa mayai(ovulation). Yai linamezwa na mirija ya falopiani iliyokaribu, kuna mirija miwili, kila mmoja una urefu wa 10sm, ambayo inaelekezwa kwenye mji wa mimba kutoka kwenye ovari.

•Kawaida utolewaji wa mayai katika ovari(ovulation) ni takribani siku 14 kabla ya hedhi yako ijayo. Muda muafaka wa utolewaji wa mayai unategemea na urefu wa mzunguko wako wa hedhi. Homoni kadhaa wa kadhaa zinafanya kazi pamoja kudhibiti mzunguko wako, kukomaa kwa mayai na muda wa kutolewa mayai (ovulation).

•Yai baada ya kutolewa huishi mpaka masaa 24 kwa wastani. Yai hili linahitaji kurutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mda huu ili mimba kutungwa.Like
Follow us .
Like
Follow us .
🇹🇿

Address


Telephone

+255653121728

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Health centertz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your practice to be the top-listed Clinic?

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram