Njombe RRH

Njombe RRH Ukurasa Rasmi wa Hospitali ya
Rufaa Mkoa wa Njombe
59017 Ramadhani -Njombe
P. O Box 1044 Njombe

Hongera Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi
17/11/2025

Hongera Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi

Hongera sana Mheshimiwa
17/11/2025

Hongera sana Mheshimiwa

Sehemu ya Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Bunge la 13 la Jamhuri ya...
14/11/2025

Sehemu ya Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo limefunguliwa rasmi leo Novemba 14, 2025.

14/11/2025

Dkt. Mercy Amos kutoka Idara ya Magonjwa ya Ndani, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe akitoa elimu kuhusu ugonjwa wa Kisukari, ikiwa ni wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza.

14/11/2025

"Ni vizuri jamii ikajenga Utaratibu wa Kuzuia Magonjwa yasiyoambukiza kuliko kutibu - Dkt. Alifa Khalid, Mtaalamu wa Magonjwa ya Dharura akitoa elimu kuhusu ugonjwa wa Shinikizo la Juu la damu.

Elimu hii ni mwendelezo wa kuadhimisha wiki ya kuzuia na kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza

14/11/2025

Tukiwa katika wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza, Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza mkoa wa Njombe, Dkt. Lucas Salatiel ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe na watanzania kwa ujumla kuachana na tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia kuongezeka kwa magonjwa hayo k**a vile tabia bwete, unywaji wa pombe kupitiliza, uvutaji sigara na ulaji usiozingatia mlo kamili.

Kwa kutambua uwepo wa Changamoto kubwa ya magonjwa hayo k**a Kisukari, shinikizo la juu la Damu, Dkt. Lucas amesema Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe katika kuadhimisha wiki hiyo inatarajia kutoa huduma katika Viwanja vya Stendi ya Zamani ya mji Njombe, kuanzia Jumatano tarehe 19 Novemba hadi Ijumaa, Novemba 21.

Wananchi watapata huduma za Vipimo na ushauri bure.

Thamini Kila Pumzi: Zuia na Tibu Nimonia Mapema, Okoa Maisha"
12/11/2025

Thamini Kila Pumzi: Zuia na Tibu Nimonia Mapema, Okoa Maisha"

28/10/2025
MADAKTARI BINGWA WA NJOMBE RRH WAANZA HUDUMA MKOBA, HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE Madaktari Bingwa kutoka Hospi...
20/10/2025

MADAKTARI BINGWA WA NJOMBE RRH WAANZA HUDUMA MKOBA, HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe wameanza kutoa huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe (Kibena) kupitia huduma Mkoba, kwa siku tatu kuanzia leo Oktoba 20 hadi Jumatano Oktoba 22, 2025.

Miongoni mwa huduma ambazo wananchi watanufaika nazo ni pamoja na Ubingwa katika Upasuaji wa Jumla, Ubingwa katika Upasuaji wa Mifupa, Ubingwa katika Upasuaji wa Pua, Koo na Sikio, Ubingwa katika Magonjwa ya Ndani, Ubingwa katika Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Ubingwa katika Magonjwa ya Watoto.

Huduma nyingine ni pamoja na Matibabu ya Macho na Huduma za Kinywa na Meno.

Mbali na Tiba, wataalamu waliopo katika Hospitali hiyo watanufaika na mafunzo mbalimbali ambayo yanalenga kuwajengea uwezo katika maeneo tajwa, pamoja na kutambua changamoto ambazo zinaweza kuhitaji mgonjwa kufanyiwa Rufaa.

Timu hiyo imepokelewa katika Hospitali ya Mji Njombe Kibena ikiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe, Dkt. Gilbert Kwesi.

Kuanzia kesho Jumatatu Oktoba 20, tutakuwepo Hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe (Kibena)Wananchi wote wenye changamo...
19/10/2025

Kuanzia kesho Jumatatu Oktoba 20, tutakuwepo Hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe (Kibena)

Wananchi wote wenye changamoto tajwa Mnakaribishwa kupata huduma hizo

Address

Mgodechi/Ramadhani Njombe Mjini
Njombe
59107

Telephone

+255678888654

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Njombe RRH posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Njombe RRH:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram