11/03/2019
*Tahadhari Kwa Wagonjwa Wa Figo:*
*1. Uhamasishaji kuhusu magonjwa ya figo na utambuzi wa mapema;*
Kuwa macho na makini ili utambue dalili za ugonjwa wa figo. Dalili za kawaida ni kuvimba kwa uso na miguu, kukosa hamu ya chakula, homa, kutapika, udhalifu, kukojoa kila mara, damu kwenye mkojo au kuwepo kwa protini kwenye mkojo. Wakati wa matatizo k**a hayo, inashauriwa kupata ushauri wa daktari ili upate upimaji wa figo.
*2. Tahadhari za kisukari;*
Kwa kila mgonjwa wa kisukari, tahadhari za kuzuia ugonjwa wa figo ni muhimu kwa sababu kisukari ndio sababu kuu ya ugonjwa sugu wa figo(CKD) na hitilafu ya figo kote duniani. Takriban asili mia 45% ya wagonjwa wapya wa hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo hutokana na kisukari. Kwa utambuzi wa mapema wa ugonjwa wa figo utokanao na kisukari njia rahisi na sahihi ni upimaji wa mkojo ili kubaini kuwepo kwa protini na msukumo wa damu kwa kila miezi mitatu. Upimaji bora zaidi wa utambuzi wa mapema kwenye kisukari ni upimaji wa maikroalbuminuria (MA) kwenye mkojo, ambao unafaa kufanywa kila
mwaka. Aidha pima kreatinini ya damu ( na e GFR) ili kuchunguza kazi ya figo angalau mara moja kila mwaka.
Msukumo wa juu wa damu, kuwepo kwa protini kwenye mkojo, kuvimba, upungufu wa sukari kwenye damu wa kila mara na kuonekana kwa dalili za kisukari kwenye jicho(diabetic retinopathy) ni vidokezo muhimu kwa figo kuhusishwa na kisukari. Jihadhari na ishara hizi hatari na upate ushauri wa daktari wako mapema.
Ili kujikinga na ugonjwa wa kisukari ya figo, wagonjwa wote wa kisukari wana wajibu wa kudhibiti kwa uangalifu sana kisukari, kudumisha msukumo wa damu uwe chini ya 130/80 mm ya Hg(ace. Inhibitor au ARB ni dawa zinazopendekezwa kwa kudhibiti msukumo wa juu wa damu) punguza kiwango cha protini kwa lishe na dhibiti mafuta.
*3. Tahadhari kwa wagonjwa wenye msukumo wa juu wa damu;*
Msukumo wa juu wa damu ndio chanzo cha pili muhimu cha ugonjwa sugu wa figo ambacho kinazuilika. Na kwa kuwa wagonjwa wengi wenye tatizo la msukumo wa damu hawaonyeshi dalili zozote, wengi husitisha matibabu kwa muda na wachache husitisha matibabu kabisa kwa kuwa wao huhisi vyema bila dawa. Lakini hii ni hatari. Msukomo usiodhibitiwa kwa muda mrefu huweza kusababisha shida na hatari k**a ugonjwa sugu wa figo , moyo kusimama ghafla na kupooza. Ili kukinga ugonjwa wa figo, wagonjwa wote wa msukumo wa juu wa damu , wanatakiwa kunywa dawa zao kila mara/kila siku, kuchunguzwa msukumo wa damu na kuwa na lishe/mlo bora na kuepuka mlo wenye chumvi. Madhumuni yawe kuweka presha /msukumo wa damu kuwa chini ya 130/80mm ya Hg. Ili kutambuwa mapema uharibifu wa figo wagonjwa wote wenye msukumo wa damu wachunguzwe mkojo na kreatinini ya damu kila mwaka.
*4. Tahadhari kwa ugonjwa sugu wa figo;*
Ugonjwa sugu wa figo hautibiki. Lakini utambuzi wa mapema na udhibiti
wa mlo,na kufuatia maelekezo ya matibabu bora itapunguza mwendelezo wa ugonjwa na kuchelewesha hatua ya matumizi ya dayalisisi au kubadilisha figo.
Udhibiti thabiti wa msukumo wa juu wa damu ni hatua muhimu ya kuzuia kwendelea kwa ugonjwa sugu wa figo . Inapendekezwa sana kuweka msukumo wa damu kuwa 130/80 mm Hg au chini. Njia nzuri ya kuthibiti msukumo wa damu ni kupima mara kwa mara hata nyumbani na kuandika sehemu ili kumsaidia daktari wako kuamua kiasi gani cha dawa akupe.
Kwa wagonjwa wenye CKD, vidokezo k**a msukumo wa chini wa damu (hypotension),kupungua maji mwilini (dehydration), kuwa na kizuizi kwenye mfumo wa mkojo (obstruction), maambukizi kwenye damu (sepsis), dawa zinazoumiza figo……nk lazima zitambuliwe. Kuchukuliwa hatua za haraka katika vidokezo hivi kunaweza kuleta nafuu kwa figo hata katika hali ya CKD.
*5. Utambuzi na matibabu ya ugonjwa wa polisistiki ya figo (PKD);*
Ugonjwa huu (ADPKD) ni hitilafu ya figo ambayo hurithiwa na hujumuisha asili mia 6-8 % ya wagonjwa walio katika dayalisisi. Mtu mzima ambaye ana historia ya ugonjwa huu wa figo yuko katika hatari kubwa sana na anastahili kuchunguzwa mapema na picha ya ultrasound ili ugonjwa ugundulike mapema. PKD haina tiba, lakini hatua k**a kudhibiti msukumo wa juu wa damu, matibabu ya maambukizi ya mfumo wa mkojo, kuthibiti lishe na usaidizi wa matibabu(supportive treatment) husaidia kudhibiti dalili, kuzuia matatizo makubwa (complications), na kupunguza kasi ya utendaji kazi wa figo.
*6. Utambuzi na matibabu ya mapema ya maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa watoto;*
Maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI) lazima uhisiwe wakati mtoto anapata baridi isiyoelezeka, kukojoa kila mara, kuchomwa wakati wa kukojoa, ukosefu wa hamu ya kula na ongezeko mbaya wa uzito.
Ni muhimu kukumbuka kuwa kila maambukizi ya mfumo wa mkojo yanapotokea (UTI), hasa yenye homa husababisha uharibifu wa figo hasa isipotambuliwa, tiba ikiwa imechelewa au kutomaliza matibabu. Uharibifu unaoweza kutokea ni pamoja na figo kuwa na makovu, figo kutokukua, msukumo wa juu wa damu, na figo kushindwa kufanya kazi baadae katika maisha. Kwa sababu hii maambukizi haya kwa watoto hayahitaji tu utambuzi wa mapema au matibabu ya haraka, bali pia tathmini makini ili kubaini vihashiria vingine, hatari au athari nyingine. Vesicoureteral reflux (VUR) ndiyo chanzo kikuu cha maambukizi haya na huleta karibu asili mia 50% ya jumla ya maambukizi yote wakati wa utoto. Ufuatiliaji ni muhimu sana kwa watoto waliopatwa na UTI.
*7. Maambukizi ya mfumo wa mkojo unaojirudia rudia kwa watu wazima;*
Wagonjwa wote wenye maambukizi ya mfumo wa mkojo yenye kujirudia rudia wanahitaji kujua sababu zake. Baadhi ya sababu ni uzibaji wa mkondo wa mkojo, tiba isiyo kamili, ugonjwa wa mawe n.k) Matatizo haya yasipotibiwa vizuri huweza kuharibu figo. Kwa hiyo utambuzi wa mapema na matibabu ya vyanzo vya tatizo kujirudia rudia ni muhimu.
*8. Matibabu sahihi ya ugonjwa wa mawe Na kuvimba kwa tezi dume (BPH);*
Wagonjwa wengi wanaouguza ugonjwa wa mawe hawana dalili zozote kwa hivyo wanakosa kugundua ugonjwa na kukosa utambuzi na matibabu yake kwa wakati/ mapema. Wanaume wengi wazee walio na tezi dume (BPH) hawatambui dalili zake kwa muda mrefu. Tatizo la mawe na tezi dume k**a hayakutibiwa mapema na kwa wakati huweza kuleta uharibifu kwenye figo. Ufuatiliaji sahihi na tiba ya wakati husaidia sana kulinda figo.
*9. Usipuuze msukumo wa damu katika umri mdogo;*
Msukumo wa damu katika umri mdogo si kitu cha kawaida na kwa hiyo huhitaji uchunguzi kamili wa chanzo chake. Magonjwa ya figo ndiyo yanaweza kusababisha msukumo wa juu wa damu kwa vijana.Kwa
kila kijana mwenye msukumo wa juu wa damu anahitaji kufanyiwa utambuzi wa magonjwa ya figo na matibabu sahihi ili kulinda figo ya mgonjwa huyu.
*10. Matibabu ya mapema ya hitilafu kali ya figo;*
Vyanzo muhimu vya hitilafu kali ya figo ni kushuka ghafla kwa utendaji wa figo. Hii utokea katika matatizo yafuatayo: kuhara, kutapika, malaria (hasa aina ya falsiparumu), maaambukizo katika damu (sepsis), madawa mengine (ACE inhibitor, NSAID’s) n.k matibabu ya mapema na bora ya vyanzo hivi huweza kuzuia hitilafu ya figo.
*11. Tahadhari kuhusu matumizi ya dawa;*
Kuwa mwangalifu. Dawa nyingi zinazonunuliwa dukani hasa za kutuliza maumivu, zina hatari ya kusababisha uharibifu wa figo hasa kwa wazee. Dawa k**a hizo zinatangazwa bila kueleza hatari zinazobainishwa kwa wanunuzi. Acha matumizi ya dawa hizi kwa mauimivu ya kichwa na mwili. Pia usijitibu mwenyewe na dawa zisizofaa. Ni vyema kupata maelezo na maelekezo ya daktari kuhusu matumizi salama ya dawa. Ni vibaya kuamini kuwa dawa zote za asili na badala (Ayurvedic medicines, Chinese herbs….nk) pamoja na virutubisho vya vyakula (dietary supplements) si hatari.
Vyuma vizito vilivyo kwenye dawa za Ayurvedic vinaweza kusababisha uharibifu wa figo.
*12. Tahadhari kwa figo moja;*
Watu walio na figo moja huishi maisha sawa na yenye afya. Kwa kuwa watu hawa hawana figo nyingine, tahadhari lazima zichukuliwe. Mgonjwa adhibiti msukumo wa damu, anywe maji mengi, awe na lishe bora, apunguze /adhibiti ulaji wa chumvi, asile vyakula vyenye viwango vya juu vya protini, na kwa namna yoyote ile azuie jeraha la hiyo figo moja. Tahadhari muhimu zaidi ni uchunguzi wa kiafya wa mara kwa mara. Inafaa amuone daktari mara moja kwa mwaka ili kuchunguza kazi ya figo kwa kuangalia msukumo wa damu, upimaji wa mkojo na damu, pia upimaaji wa ultra sonogramu ,iwapo inahitajika.
*TUKUMBUKE SIKU ZOTE KINGA NI BORA KULIKO TIBA, K**A UNAYO TATIZO USISITE KUULIZA TUKAKUSAIDIA KWA UELEWA ZAIDI NA USHAURI PIA NI JINSI GANI UNAWEZA UKAJIKINGA AU K**A UPO HATUA ZA AWALI, UFANYE NINI ILI UWEZE KUONDOKANA NALO.*
*KARIBUNI SANA....... Tuwasiliane hapa kwa maelekezo na maswali zaidi au piga namba 0764899798.*