27/02/2026
Girfe Oscar ni kijana wa miaka 22 kutoka Kijiji cha Ituwa, Mkoa wa Mbeya anaishi na tatizo la mtindio wa ubongo (cerebral palsy), hali iliyoaathiri utendaji wa viungo vya mwili wake hususani mikono, na pia hawezi kuongea Lakini Oscar ana akili nzuri sana, anajifunza kwa wepesi, na ana ndoto kubwa kielimu.
Huyu ni mhitimu wa elimu ya msingi mwaka 2024 na sasa anasoma kidato cha pili (secondary school) lakini Kwa miaka yote saba aliyosoma elimu ya msingi, hakuweza kushika kalamu wala kuandika darasani kwasababu hawezi kutumia mikono yake vizuri.
Mnamo mwezi Oktoba 2024, wazazi wake walimleta hapa INUKA REHABILITATION HOSPITAL, wakiwa na tumaini moja tu ya kwamba mtoto wao ajifunze kuandika.
Akiwa Inuka, wataalamu walibaini kuwa anaweza kuandika kwa kutumia kichwa kupitia vifaa maalumu ambavyo ni (kompyuta mpakato, kiti na meza maalumu pamoja na head pointer) ilivyo bahati mpango huo ulifanikiwa na sasa Girfe anaendelea na masomo yake ikiwa tatizo la kuandika limetatuliwa.Kwa mara ya kwanza maishani mwake, aliweza kuandika mwenyewe na alifurahi sana, yuko tayari kujifunza, kushiriki darasani, na kutimiza ndoto zake.
Hadithi ya Girfe inatufundisha jambo moja muhimu sana ya kwamba Ulemavu si kushindwa. Kwa msaada sahihi, kila mtoto anaweza kutimiza ndoto zake.
……….......................................................................................................................
Girfe Oscar is a 22-year-old student from Ituwa Village in Mbeya Region living with cerebral palsy. The condition affected his body movement, especially his hands, and he is unable to speak yet his intellectual ability is strong and remarkable.
For seven years in primary school, Girfe never held a pen or wrote in class because he could not use his hands. Still, he completed primary education in 2024 and now studies in secondary school.
In October 2024, his parents brought him to INUKA Rehabilitation Hospital with one hope that he could learn to write.
After assessment, specialists introduced him to assistive technology: a laptop, an adapted chair and desk, and a head pointer, for the first time in his life, Girfe wrote independently.
Today, he continues his studies with confidence and dignity.
His story reminds us of one powerful truth with the right support; every child can achieve its dreams.