
20/06/2025
Dalili za presha ya kupanda zinaweza zisiwe za wazi sana, ingawa ni muhimu kuzifahamu.
Ni muhimu kuelewa kuwa presha inaweza kuwa kubwa bila kuonesha dalili yoyote, hivyo ni muhimu kufahamu presha yako mara kwa mara ili isikuletee madhara.
Kutokuwa na dalili mahususi, presha ya kupanda ndiyo maana ikaitwa muuaji wa kimya kimya.
Dalili za presha ya kupanda zinaweza kuwa kali au za kawaida kulingana na upandaji wa presha.
Hivyo tegemea dalili tofauti presha inapopanda kidogo, presha inapopanda katika kiwango cha tahadhari (hypertension urgency), na presha inapopanda kiwango cha hatari (hypertension emergency).