29/04/2021
Unapomwambia mtu ajitahidi awe k**a fulani,je wamjua vizuri huyo fulani? Je wayajua yote yanayomuhusu ambayo yapo sirini na hajawahi kuyaweka hadharani? Jitahidi uwe k**a Baraka Frances,ivi wewe huyu Baraka unayetaka niwe k**a yeye unamfahamu kiundani kweli? Au unazuzuka tu na unachokiona mtandaoni? Ivi unajua kwa nini yupo ivyo alivyo? Je,upo tayari kukinywea kikombe alichokinywea yeye? Je, ni uzuri wa sura yake au uzuri wa kamera anayotumia? ASIJE HUYU MTU UNAYEMSISITIZA awe k**a fulani akawa kweli k**a huyo fulani kisha ukashindwa kustahimili huo ufulani uliokuwa ukiusisitiza pasipo kuujua undani wake.
1. Mkubali mtu jinsi alivyo,pasipo kumfananisha na fulani. Chungwa na embe yote ni matunda na yote yana umuhimu mwilini mwako. Tafuta thamani ya mtu,usitafute udhaifu wake.
2. Kuwa wewe hivyo unavyotaka mwenzako awe. K**a hawezi jifunza toka kwako hataweza kujifunza toka kwa fulani.
3. Jikubali ulivyo pasipo jilinganisha na fulani. Kuna zaidi ya ukionacho.
4. K**a aliyekuumba alikuumba kwa mfano wake, ya nini kujitaabisha ufanane na mwingine tena? Respect that, remain original and true to yourself.
Amka Awareness Clinic
Baraka Frances - watsapp +255715439205
JE, NA SISI WABADILISHA WATU TABIA TUFANYEJE BAADA YA KUYASIKIA HAYA?
1. Msiwabebeshe watu mizigo ambayo ninyi wenyewe hamuwezi kuibeba mkivaa viatu vyao. Watu huona nuru wakaifuata na sio nuru huona watu ikawalazimisha waifuate.
2. Wekezeni katika upendo,kwani upendo huushinda wingi wa dhambi. Na upendo ni pamoja na matendo sio kauli pekee.
3. Kila unayemuona anafanya usichokipenda ana sababu nyuma yake.
K**a unamwambia mtu aache kudokoa chakula wakati haumpi icho chakula, basi jua ataacha ukiwepo na atadokoa ukiondoka,na usipoondoka atadokoa kwa majirani, kwa kuwa kauli yako haijaondoa NJAA tumboni mwake. (Watu watatafuta mbinu za kuikwepa sheria,na sio kukwepa kutenda makosa ikiwa sababu ya kutenda hayo makosa haijaondolewa)
4. Siku mkijifunza kuacha kuwahukumu watu na kuanza kujifunza kuwaelewa watu mtafunguliwa macho toka katika upofu huu mkuu zaidi ya ule wa Bartholomayo.
Ramadan Kareem