11/03/2023
SUKARI INAUA MFANO WA SIGARA.
Na Mfamasia wako: Mohammed Hamid.
Uvutaji wa sigara ni mbaya kiafya, lakini ulaji mwingi wa sukari una athari inayofanana. Unaharibu kabisa viungo muhimu vya mwili mfano wa moyo na ini .
Kwa mujibu Shirika la Moyo la Marekani mwanamke anapaswa ale vijiko vya sukari visivyozidi sita kwa siku, na mwanamme asizidishe vijiko nane kwa siku. Lakini uhalisia unaonesha watu hunywa zaidi ya wastani wa vijiko 40 vya sukari kwa siku pasina kujijuwa. Unga wa kahawa, soda pamoja na juisi nyingi za matunda za viwandani zimebeba sukari nyingi. Vinywaji vya kuongeza nguvu (inaji) ndio havisemeki kabisa kwa kubeba sukari nyingi na isiyo salama. Vinaweza kukuua mapema zaidi ya sigara.
Ulaji wa sukari uliokidhiri unaweza kusababisha maradhi ya moyo na mfumo wa damu. Maradhi ya moyo na damu yanaongoza kwa kuuwa idadi kubwa ya watu duniani kuliko maradhi mengine yoyote.
Kwakuwa sukari huhifadhiwa mwilini k**a mafuta. Ulaji wa sukari uliokidhiri husababisha uzito/ kitambi. Ripoti kutoka shirika la uingreza linalojihusisha na kansa linasema kadri uvutaji wa sigara unavyokuwa mdogo, uzito uliokidhiri unazidi miongoni mwa watu. Ifikapo mwaka 2043 uzito uliokidhiri unategemewa kuupita uvutaji wa sigara kwa kuongoza kusababisha kansa uingreza.
Tahadhari chukuwa hatua na mapema.
Usinywe vinywaji vilivyobeba sukari nyingi na fanya mazowezi kuondoa sumu mwilini. Na nitafute inbox kwa ushauri wowote wa kiafya.
Mohammed Hamid