06/12/2023
Watu wengi leo wamefumbwa hata hawajui lipi liwapasalo kufanya Kwa wakati. BIBLIA Inasema katika Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokua mzee. Leo Wazizi wame lichukulia andiko hilo kimwili na kufanya Mtoto awe na uelewa mkubwa kwa mambo ya kidunia Mungu Kwa kutupenda alituletea Katiba yake ili tuifuate! kutoka 20:2 -17 Huo ndio muongozo ambao mwanadamu lazlma aufuate na kuufundisha kwa Watoto Vijana na Wazee!. Hasa kuweka mkazo katika kuwafundisha Watoto.Yesu ambae ni Mwana wa Mungu, aliifafanua nakuiweka Katika sehemu mbili Sehemu ya kwanza ina muhusu Mungu na sehemu ya pili inamuhusu Mwanadamu kumbuka kua sehemu ya Mungu ndio ya Kwanza hivyo ilipaswa Watoto watiliwe mkazo Katika kuwafundisha Mambo ya Mungu wawe na uelewa zaidi ya Mambo ya kidunia. Marko 12 :17 Leo Wazazi mlipo kosea mmeshikilia upande mmoja. Nandio maana Vitoto vingi leo viki inukia kidogo tabia zao wanakosa kicho cha Mungu! Kizazi kinacho kuja Watu watakua hawamjui Mungu !!Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? kwakutii akilifuata neno lako. Zaburi 119 :9 (Yoshua 1 :8. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyo andikwa humo; maana ndipo utakapo ifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapo sitawi Sana!. (Fumbua Macho Yako Mwanadamu)