Dr. Amar

Dr. Amar Good Health is a life Wealth.

KaribuSasa tumehamia TikTok, maswali na majibu yote kuhusu dawa, tiba n.k utayapata live na kwa muda sahihi.Follow
11/04/2024

Karibu
Sasa tumehamia TikTok, maswali na majibu yote kuhusu dawa, tiba n.k utayapata live na kwa muda sahihi.

Follow

0 Followers, 11 Following, 0 Likes - Watch awesome short videos created by Amar

Kwa wanaosumbuliwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa karibuni sana. Follow Kisha nitakuona na tuanze utatuzi wa haraka ...
13/07/2023

Kwa wanaosumbuliwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa karibuni sana.
Follow Kisha nitakuona na tuanze utatuzi wa haraka kwa 100%

UHUSIANO KATI YA DAMU NA TABIAJe unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?Kwa kawaida kila binadamu...
15/04/2023

UHUSIANO KATI YA DAMU NA TABIA

Je unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu?

Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O.

Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” k**a ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko wenye vyanzo vingine. Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea,

kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula. Baadhi ya watafiti nchini korea wamebainisha kuwa hata namna tunavyopendelea kuketi hutegemea sana na makundi yetu ya damu, sasa tuangalie uhusiano huu

Damu kundi “A”

Hawa watu maranyingi huwa mifano ya kuigwa na wengi kwasababu ya kiu zao na upiganaji wao kwenye mafanikio, ni watu wema,wapole na wenye tabia njema. Pamoja na hayo ni rahisi sana watu hawa kupata msongo wa mawazo “stress” na kufikiria sana vitu. Wakiamua kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mtu basi wanazama kabisa na wanaweza hata kujisahau wao.

Mazuri yao

Ni watu wanaopenda vitu vikamilike katika hali ya juu “perfectionists”, wanapenda mpangilio maalumu, wanapenda na wanaweza kuchambua mambo sawia, wanawajibika na kubeba majukumu yao,wana huruma na wako tayari kusaidia, waaminifu, ni wagunduzi, wanamaanisha, wavumilivu, na wenye tabia njema.

Mapungufu yao

Wasumbufu,wana hisia kali hata kwenye vitu vya kawaida, wakitaka kitu wametaka, wengine wana aibu,wengine wakimya zaidi na wanaopenda kujichanganya.
Kwenye maisha ya kijamii
Ni mtu ambaye unaweza kumwamini na kumtegemea
Anajali na kumaanisha
Wakati wote huepuka shari,misuguano na magomvi
Maranyingi hawapendezwi wala kufurahia sherehe zenye makelele na shangwe za ajabu ajabu,wanapendelea ukimya na utulivu.
Kazini
Unaweza kumwamini na kumtegemea katika majukumu
Wanapenda ufanisi wa kiwango cha juu kwahiyo kazi zao mara nyingi ni bora sana.
Bahati mbaya wanajali sana hata vitu vilivyo vidogo nahii huwafanya kuwa na msongo wa mawazo kirahisi.
Wasio waelewa vema watu wa kundi hili wanaweza kupata shida kufanya nao kazi
Kwenye mahusiano na mapenzi
Ni ngumu kidogo wao kufunguka na kushirikisha mambo yao.

Wanaweza kuonekana wenye aibu, au waoga.
Ukitaka kumchumbia au kuchumbiwa na mtu wa kundi ‘A’ unahitaji uvumilivu.
Wakiamua kupenda utawafahamu wakati wote na ingawa watakuruhusu ufahamu tu yale maeneoa ya maishani mwao ambayo wanajua unahusika, hawawi wazi katika kila eneo.
Ukweli mwingine kuhusu watu wa kundi ‘A’
Ni watu wabunifu na wenye ujuzi wa usanii “artists”
Wanalewa kirahisi sana, kilevi kidogo tu kitampelekesha sana
Wengi wao hupendelea kula mboga mboga “vegetarians”

Damu kundi “B”

Watu wa kundi hili maranyingi ni wenye tabia za kuasi na ni ngumu kuwazuia au kuwatuliza. Wanandoto na maono makubwa,wanasukumwa kwa kasi na kiu zao ingawa wanaweza kuwa wakali na wasumbufu na mara nyingine ngumu kukaa na kuzoeana nao. Wanakisimamia sana kile wanachokiamini hata k**a ulimwengu mzima usimame kinyume nao.

Mazuri yao

Wanasukumwa katika kufikia malengo yao, wako kasi kiutendaji,wanapenda raha,wana hisia nzito , wanayatazama maisha katika mtazamo chanya , wanaweza kujisimamia na kujitegemea na hawahitaji ushirika au kukubaliwa na wengine.
Mapungufu yao
Wabinafsi sana,mara nyingine wanakwepa majukumu yao,wagumu sana kusamehe,wasumbufu,wanaweza kuwa wakatitili na wenye hasira za haraka.
Maisha yao kijamii
Maranyingine ni ngumu kushirikiana nao au kuwa nao maana wanapenda kufanya mambo yao wenyewe.
Kazini
Ingawa wanaweza kuwa na malengo mengi na maono pia lakini wanaweza kuwa wasumbufu na wagumu katika kushirikiana nao kazini. Ni ngumu kufanya nao kazi maana wanataka kufanya pekeyao.
Mahusiano na mapenzi
Unaweza kufurahi nao sana kwenye mapenzi lakini uwe tayari kuvumilia hasira zao kali na za ghafla. Vumilia hali yao ya kukwepa majukumu pia,fahamu kuwa wanaweza kuwa wakali, wakatili na wasio maanisha kile wanachokisema.

Baadhi ya ukweli wa kitafiti kuhusu watu wa kundi B.

Wanatabia ya utukutu.
Pamoja na baadhi ya mazuri yao bado wanaweza wasiwe watu wazuri kwenye kuwa mume, au kuwa wapenzi wazuri kwa wasichana wao. Hii ni kutokana na urahisi wa tabia za kukosa uaminifu kimapenzi na urahisi wa kuumiza mioyo ya wengine.
Wanatabia ya kupenda wanyama “they love pets”
Wana kinga kubwa na imara ya mwili katika kujikinga na magonjwa.
Wanafurahia zaidi vyakula vitokanavyo na wanyama k**a vile maziwa “dairy products” n.k

Damu kundi “AB”

Kundi hili ni watu wenye haiba mchanganyiko, hawa huwa na tabia tofauti kuanzia kuwa waoga na wenye aibu hadi wengine ni wapenda mitoko na wacheshi,wako wanafanya mambo kwa kuongozwa na mawazo na wengine hawawazi kabisa kile wanacho taka kukifanya,hii inafanya watu wa kundi hili kuwa watu wa kushangaza sana mara unapokuwa nao.

Mazuri yao

Ni rahisi sana kuwa rafiki nao.
Wanachukuliana na mazingira haraka na kwa urahisi.
Wenye kufurahisha unapokuwa nao ingawa ni watu wasiotabirika.
Wana mawazo,wana akili sana,hupenda kuweka mambo yao kwa vitendo na pia huongozwa na misimamo ya kifikra.

Mapungufu yao

Wagumu katika kufanya maamuzi.
Wanasahau sana
Ni wenye hisia za kayumba “mood swing”, mara wana furaha mara wamekasirika.
Sio waaminifu.
Ni wapinzani,wabishi na wakosaji.
Ni watu wabinafsi.

Maisha ya kijamii

Wanaweza kuwa marafiki wazuri na wenye kufurahisha.
Maongezi yao ni yenye kuhamasisha nayenye akili na kufikiria kwa hali ya juu.
Kwa kutokuwa wenye kutabirika, wengine huhofia kuumizwa kihisia au kukatishwa tamaa au kuumizwa moyo na watu hawa, hususani pale wanapokuwa sio waaminifu.
Kazini
Wanaweza kuwafurahisha na kuwapa burudani mnapofanya kazi nao lakini sio watu wa kuwategemea sana,wanaweza kukuangusha kirahisi.

Mahusiano ya mapenzi

Kuwa katika mahusiano na mtu wa kundi la damu la AB kunaweza kuwa kwenye kufurahisha,unaweza usiwena nyakati nyingi za upweke. Pamoja na haya fahamu kwamba watu hawa wanaweza kuwa wabishi na wakosoaji na maranyingine maneno yao yanaumiza. Mpenzi wa mtu au watu wa hivi lazima aelewe jinsi hisia zao zilivyo na zinavyobadilika mara kwa mara,na pale inapobidi basi uwetayari kuwapa nafasi wanayostahili ili usijiumize sana.
Baadhi ya ukweli wa kiutafiti kuhusu watu wa kundi hili.
Ni watu wazuri kwenye mambo yahusuyo fedha.
Maranyingi wanajihusisha na wanaopendendelea shuhuli za kisanaa au mambo yenye sanaa ‘arts’
Ni watu wanaoaminika kuwa wabinafsi zaidi hata katika uchangiaji wa damu,watu hawa wanaweza kupewa damu na mtu mwingine yeyote ila wao hawawezi kumpa damu yeyote isipokuwa mwenzao wa AB.
K**a walivyo watu wa kundi ‘A’ na kundi ‘B’,watu wa kundi la damu ‘AB’ hupendelea vyakula vya mboga mboga “vegetables” na pia vyakula vitokanavyo na wanyama “dairy products”

Kundi la damu aina ya O.

Hawa maranyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote. Sio wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana naya wazi, sio wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.

Faida zao

Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidii, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuonamambo hata kabla hayajatokea,wanakiu ya kufahamu na kudadisi na pia niwatu wema na watoaji.

Mapungufu yao

Maranyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu,unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na nirahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.

Maisha ya kijamii

Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi,ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.
Kazini
Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tamaa na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayo fanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe..

Mahusiano ya mapenzi

Ni watu wenye mvuto wa kimahaba pia watu hawa wana hisia Kali za kimapenzi wanaweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.

Ukweli wa kitafiti kuhusu watu hawa

HAWAPATI MARADHI KIRAHISI
Kwanza ifahamike kuwa watu wenye damu kundi hili wamegawanyika mara mbili ambazo ni damu kundi “O” chanya (O positive) na kundi “O” hasi (“O” negative) mgawanyo huu umetokana na mgawanyo wa kitaalamu ambao huitwa “rhesus factors” ambao ndio unaotumika kugawanya makundi ya damu.
Kwa ujumla kundi hili la damu liwe hasi au chanya halina proteins maalumu zilizomo ndani ya damu ambazo huitwa “antigens” ambazo ndizo mara nyingi ni rahisi kushika magonjwa isipokuwa lina “antibody” ambazo ndizo kinga mwili zinazopambana na maradhi ndiyo maana damu kundi “O” linaitwa “Universal Donor” damu kundi lolote linapokea.
Na kwa wakati fulani maradhi yanayowasumbua watu wenye damu kundi hili ni malaria, kichwa na mafua na wengine husumbuliwa sana na ugonjwa wa kutoka damu za pua (Rhinits) au wengine huita kambaku ambao husababishwa na kula nyama yenye lehemu nyingi (cholestrolel) ambazo ni nyama ya ng’ombe, kondoo, samaki aina ya dagaa, uwono na mboga ya majani inayoitwa kisamvu na wakati mwingine maziwa ya ng’ombe au kutembea kwenye jua kali sana au kutumia manukato yenye harufu kali.

NI WAPENDA NGONO

Watu wenye damu kundi hili wana hisia kali sana za mapenzi hii ni kutokana wana homoni nyingi, hali hii inawapelekea kupenda sana ngono na vile vile huwa wakizaa wanafanana sana na watoto wao iwe sura, tabia au mwendo iwe mwanamke au mwanaume
Watu hawa Mara nyingi huwashwa masikio yao kwa ndani hivyo Mara nyingi wanajikuna masikio
Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi.
Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo.
Wanaaminika kuwa watu wema na waliotayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote.
Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama “meet lovers"

Pelvic inflammatory disease (PID) is an infection of the female reproductive organs. It most often occurs when s*xually ...
29/01/2023

Pelvic inflammatory disease (PID) is an infection of the female reproductive organs. It most often occurs when s*xually transmitted bacteria spread from your va**na to your uterus, fallopian tubes or ovaries.

In most cases, the condition is caused by a bacterial infection spreading from the va**na or cervix (entrance to the womb) into the womb, fallopian tubes and ovaries.

PID is often caused by more than one type of bacterium and it can sometimes be difficult for doctors to pinpoint which are responsible.

This means a combination of antibiotics will be prescribed so a variety of bacteria can be treated.

Sexually transmitted infections (STIs)
The main cause of PID is through a s*xually transmitted infection (STI) such as chlamydia, gonorrhoea or mycoplasma genitalium.

These bacteria usually only infect the cervix, where they can be easily treated with antibiotics.

But if they're not treated there's a risk the bacteria could travel into the female reproductive organs.

If you have chlamydia and it's left untreated, it may develop into PID within a year.

Other causes of PID
In many cases, the cause of the infection that leads to PID is unknown.

Sometimes, the usually harmless bacteria found in the va**na can get past the cervix and into the reproductive organs.

Although harmless in the va**na, these types of bacteria can cause infection in other parts of the body.

This is most likely to happen if:

you have had PID before
there's been damage to the cervix following childbirth or a miscarriage
you have a procedure that involves opening the cervix (such as an abortion, inspection of the womb, or insertion of an intrauterine device (IUD)
Which areas can become infected?
If an infection spreads upwards from the va**na and cervix, it can cause inflammation of the:

womb lining (endometrium)
fallopian tubes
tissue around the womb
ovaries
lining of the inside of the abdomen (peritoneum)
Pockets of infected fluid called abscesses can also develop in the ovaries and fallopian tubes.

Who's most at risk?
Anyone with female reproductive organs can get PID, but you're more likely to get it if you:

have more than 1 s*xual partner
have a new s*xual partner
have a history of STIs
have had PID in the past
are under 25
started having s*x at a young age

SABABU ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUMEZifuatazo ni sababu kuu zinazopelekea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume...
14/01/2023

SABABU ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Zifuatazo ni sababu kuu zinazopelekea tatizo la upungufu wa nguvu za kiume :

Magonjwa:
Magonjwa k**a vile kisukari, shinikizo la damu, kupooza kwa mwili (paralysis) n.k.

Umri mkubwa:
Wazee wenye umri mkubwa ni waathirika wakubwa wa tatizo hili.

Sababu za kisaikolojia (Emotional reasons)
Msongo wa mawazo (stress & depression), hasira na huzuni huchangia tatizo hili kwa kiwango kikubwa.

Vyakula:
Vyakula vya kemikali k**a vile soda na vyakula vya mafuta pia sukari huchangia kwa upande mwengine utumiaji wa vyakula vya asili na matunda k**a vile parachichi pamoja na unyawaji wa maji ya kutosha huimarasha siha na kukupa matokeo mazuri kwenye tendo la ndoa.

Pombe na uvutaji wa sigara
Kotokufanya mazoezi
Athari zinazotokana na madawa ya kemikali
Matatizo ya Majini (Mahaba):
Majini Mahaba humuingia mwanaadamu kwa lengo la kufanya nae mapenzi,

k**a alivyo binaadamu wa kawaida majini wana wivu, kutokana na wivu humdhoofisha muathirika ili asifanye mapenzi na mtu mwengine.

Kuangalia picha za uchi (X) pia kuangalia wanawake walio vaa utupu
Punyeto
Kuwa bize sana kimwili na kiakili
K**a unahitaji dawa ya asili ambayo itakusaidia kumudu Hadi dakika 40 njoo Whatsapp

Gharama ni Tsh. 30,000/- tu.
Uhakika 💯

Pia nifollow https://www.facebook.com/Hamy.Namawala?mibextid=ZbWKwL upate post mpya zaidi

Tatizo La Mwanamke Kukosa Hamu Ya Kufanya MapenziTatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi au kukosa nyege kwa lugha ya m...
31/08/2022

Tatizo La Mwanamke Kukosa Hamu Ya Kufanya Mapenzi
Tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi au kukosa nyege kwa lugha ya mitaani huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume lakini ni wanaume wanaokerwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake. Wakati ambapo ni asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni mara mbili ya hii ya wanaume. Lakini wakati ni asilimia 23 ya wanaume wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.
Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa sababu kuna mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana na hili tatizo.
Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalibali yanayomtokea katika maisha yake. Baadhi ya matukio yanayoathiri hamu ya mwanamke kufanya mapenzi ni pamoja na kuanza na kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme, kupata ujauzito, na magonjwa. K**a wewe mwanamke umepatwa na hali hii unaweza kukabiliana nayo kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayobadilisha hali hii au kutumia baadhi ya dawa zinazosaidia kuondoa tatizo hili.
Jee, Utajuaje k**a Una Tatizo?
Kuna vitu vingi ukiviona vinakutokea, ujue una tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Tulivijadili viashiria hivi kwa kina tulipozungumzia tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanaume.
Sababu Za Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa
Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika makundi manne:
1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme
Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na k**a atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.

2. Matatizo Katika Maisha Yako
Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:
MATATIZO KATIKA KUFANYA TENDO LA NDOA.
K**a mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au k**a mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.
Matatizo ya afya
Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis), kansa, ugonjwa wa kisukari, high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili.
Matumizi ya madawa
Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.
Mtindo wa maisha
Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.
Upasuaji
Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneo ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.
Uchovu:
Unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.

3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni.
Kukoma hedhi: Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.
Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

4. Matatizo Ya Kisaikolojia
Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:
• Wasiwasi na kuwa na msongo wa mawazo
• Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
• Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
• Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia k**a kupigwa au kubakwa
• Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi
Njia Za Kuondoa Tatizo La Kukosa Hamu Ya kufanya Tendo La Ndoa

Hakuna dawa ya moja kwa moja toka hospitalini kwa sasa hivi kwa ajili ya kuondoa tatizo hili, hata hivyo wanawake wengi wanaweza kurudi kwenye hali zao za kawaida kwa kushirikiana na waume zao waelewa. Jaribu kufanya mambo tuliyoyadokeza katika mada yetu ya “Mwanamme Kukosa hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa” ukisaidiana na mumeo. Unahitaji kuchunguza taratibu na kwa kina chanzo cha tatizo lako, na taratibu lifanyie kazi kwa msaada wa mume wako.
Katika nchi zilizoendelea, kila siku wamekuwa wakija na dawa na vifaa vipya vya kuondoa tatizo hili na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida. Vipo ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni Suction Vi*****rs, Desire Creams na Er****on Drugs.
Unaweza kupata mafanikio makubwa (wasomaji wangu wengi wamefanikiwa na kunishukuru) kwa kutumia chakula kinachosaidia kuongeza hamu au kwa kutengeneza na kutumia vi**ra asilia. Hivi nimevielezea hapa chini. K**a hivi bado havijakusaidia, nashauri utumie virutubishi vya mwili ambavyo husamabazwa na makampuni mbalimbali. Vipo vinavyofanya kazi kwa haraka na kutibu kabisa tatizo hili. Endapo umepata tatizo kutambua virutubishi vizuri vya kutumia, wasiliana nasi kwa kutumia njia yo yote iliyo rahisi kwako kati ya hizi nilizoziorodhesha chini ya ukurasa huu.
Chakula Cha Kuongeza Hamu Ya Mapenzi

Utafiti umeonyesha pasi shaka kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi. Baadhi ya chakula na virutubishi vimehusishwa na hamu ya kufanya mapenzi (nyege). Virutubishi ndani ya chakula ambavyo vinasaidia hali hiyo ni antioxidants, vitamin C, vitamin E, potassium na zinc. Kirutubishi cha zinc ambacho hupatikana ndani ya vitunguu swaumu, mbegu za maboga, ufuta na mbegu za matikitimaji, kinaongeza mbegu kwa mwanamme (s***m count) hivyo humsaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Chakula cho chote chenye virutubishi hivi kikiliwa, humfanya mlaji asikie hamu ya kufanya mapenzi au kwa maneno ya mtaani, chakula hiki kinasaidia kuongeza nyege. Baadhi ya chakula cha kuongeza nyege ni:
Tikitimaji-Hili linachukuliwa kuwa ndilo tunda bora katika kuboresha afya ya mapenzi. Tunda hili lina asilimia 92 ya maji na asilimia 8 zinazobakia zina phytonutrient citrulline ambayo hugeuzwa kuwa arginine. Arginine ni amino acid ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa kwenye hali ya ubora wake na kusadia damu kupita vizuri zaidi. Tikitimaji kwa hiyo husaidia damu ifike kwa kiwango kizuri zaidi kwenye sehemu ambazo hutakiwa kutanuka wakati mtu akipata hisia za kufanya tendo la ndoa ambazo ni viungo vya ndani ya kisimi cha mwanamke na ndani ya uume wa mwanamme.

Strawberries– matunda haya yana antioxidants kwa kusaidia afya ya moyo na mishipa ya damu (arteri) na vitamin C ambayo huongeza kiwango cha mbegu kwa mwanamme.
Pombe-glasi moja ya mvinyo hukufanya uwe na akili tulivu. Pombe kwa kiwango kikubwa huleta kinyume cha matarajio na kuondoa kabisa hamu ya mapenzi.
Avocadro-tunda hili lina vitamini E ambayo ni antioxidant. Ndani ya tunda hili kuna potassium na vitamini B6 ambavyo huboresha afya ya moyo na kusaidia mzunguko wa damu.

Viazi vitamu-hivi vina potassium ambayo husaidia kuondoa tatizo la high-blood pressure.
Chakula kingine katika kundi hili ni broccoli (picha hapa chini), karafuu, mayai na tangawizi.
Kuna mchanganyiko wa matunda ukisagwa pamoja na kunywewa umeonyesha kuongeza hamu ya kufanya mapenzi au kuongeza nyege. Nilionyesha namna mbili za kutengeneneza mchanganyiko huo na nikauita “Vi**ra asilia.” Nitaongeza mchanganyiko wa tatu wenye matunda mengi zaidi ili uweze kuchagua ule utakaoona ni rahisi zaidi kuutengeneza.
Jinsi Ya Kutengeneza Vi**ra Ya Asili
Kusanya matunda k**a yanavyoonyeshwa kwenye video hii hapa chini, saga kwa pamoja katika blender na kisha kunywa glasi moja ya mchanganyiko huo. Hakuna kipimo kamili cha kutumia, lakini ukipata glasi tatu kwa siku utapata mabadiliko ya kutosha kabisa. Wapo watu wengi waliofuata ushauri huu, wakanipigia simu kuwa hali zao zimekuwa nzuri sana baada ya kutumia kinywaji hiki. Jaribu kisha nipe matokeo.
K**a umeshindwa kupata matunda yote kwa kutengeneza vi**ra hii asilia, nenda ukurasa wa “Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa” ambamo nimeelezea vi**ra asilia ya matunda mawili tu, tikiti maji na limau.

K**a una swali lolote au maoni yako kuhusiana na mada hiyo hapo juu, usisite kutuandikia. Pia usisite kuomba ushauri zaidi pale ulipojaribu njia hizi ukakwama mahali.

09/07/2022
MAMBO YA KUZINGATIA KWA WAGONJWA WOTE WA FANGASI. Kwa mgonjwa wa fangasi sugu unaweza kujikinga kwa kuepuka mambo mbalim...
28/06/2022

MAMBO YA KUZINGATIA KWA WAGONJWA WOTE WA FANGASI.

Kwa mgonjwa wa fangasi sugu unaweza kujikinga kwa kuepuka mambo mbalimbali na kuzingatia kanuni ya afya na usafi.

1. Vaa nguo za ndani ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au Hariri

2. Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya mpaka pale atakapotibwa na kupona kabisa.

3. Usifanye ngono kwa mdomo (oral s*x)

4. Kula mlo wenye virutubisho muhimu.

5. Tumia baadhi ya viungo k**a kitunguu saumu, mdalasini na manjano,vinasaidia kupambana na fangasi

6. Punguza matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye sukari

7. Epuka kuoga maji ya moto sana (hot baths) tumia maji ya uvuguvugu

8. Mafuta ya n**i yana uwezo mkubwa katika kupambana na fangasi kutokana na uwepo wa viambata hai vya lauric acid na caprylic acid.

Tumia kwa kupakaa eneo lililoathirika na pia kupikia kwenye chakula. Hakikisha unapata mafuta asili yasiochanganywa na kemikali.

Baada ya wateja wengi kufanikiwa kupitia ukurasa huu Sasa utaanza kulipia huduma.

Kwa gharama ya Tsh. 5,000 za kitanzania utapatiwa huduma zifuatazo
1. Kuhojiwa historia ya ugonjwa wako
2. Kupewa ushauri pamoja na kuelekezwa dawa halisi ya ugonjwa wako.
3. Kufuatiliwa kwa karibu juu ya maendeleo ya mgonjwa.

NB. Dawa utanunua mwenyewe baada ya kuelekezwa.

Baada ya kulipia huruma utaunganishwa kwenye Group la ushauri na Tiba ili uweze kupata tips mbalimbali za Afya na Tina.

Karibuni sana.

https://chat.whatsapp.com/Kyr8MwwTKnp5g3rqe0DBH0

Karibu nawe nikusaidie. K**a unateseka na magonjwa mfano P.I.D, FANGAS, MIWASHO SEHEMU ZA SIRI, MAUMIVU WAKATI WA TENDO ...
19/05/2022

Karibu nawe nikusaidie. K**a unateseka na magonjwa mfano P.I.D, FANGAS, MIWASHO SEHEMU ZA SIRI, MAUMIVU WAKATI WA TENDO N.K. Wasiliana na mimi tafadhali.

Wengi huachana na wenza wao sio kwa sababu upendo umeisha bali ni kutokana na sababu nyingine tuu.Labda unateseka sana n...
25/04/2022

Wengi huachana na wenza wao sio kwa sababu upendo umeisha bali ni kutokana na sababu nyingine tuu.

Labda unateseka sana na unajutia muda ulio poteza. Unapata wakati mgumu kusahau yote mliyo share pamoja na kila unapo kumbuka basi maumivu yanakuzidi.

Yawezekana pia bado mnawasiliana na inafika wakati pia anataka mkutane kimwili wakati yeye tayari ana mahusiano mengine.

Unabaki njia panda bila kujua nini cha kufanya huku huzuni ikiwa umekujaa, hofu ya kuanza upya imekutawala, imani ya kumuamini mtu mwingine imepotea na pia upweke pamoja na maumivu vinakuandama kila kukicha.

Unahitaji kujua jinsi ya kuanza upya na kuweza kusahau yaliyo pita na sio usonge mbele huku mapito yakikurudisha nyuma kila siku. Inawezekana kabisa kua sawa tena na kua bora kuliko hata mwanzo.

Ni suala la kujua unaanzaje kwenye safari ya kutimiza malengo yako.

Karibu Whatsapp 0654028112
Kwa ushauri, Tiba na muongozo mzuri wa kisaikolojia karibu sana Huduma zangu ni mzuri na hakika unaenda kuimarika katika maisha yako. Hakuna huduma za bure kwa njia ya Private 🙏.

NINI CHA KUFANYA K**A MWANAUME WAKO AMEANZA KUBADILIKA?Ukiona mwanaume kabadilika, hapigi simu k**a zamani basi kitu kik...
26/03/2022

NINI CHA KUFANYA K**A MWANAUME WAKO AMEANZA KUBADILIKA?

Ukiona mwanaume kabadilika, hapigi simu k**a zamani basi kitu kikubwa na chamuhimu zaidi ni kumpa nafasi, yaani kuacha kujaribu kummiliki na kumuacha akukumbuke. Mwanaume hawezi kukukumbuka wala kukumiss k**a unampigia sumu mara 10 kwa siku.

K**a unatuma meseji 20 ambazo hazijibiwi, k**a kila siku unakazania kwenda kwake mpaka yeye ndiyo anakuambia yuko bize! Najua unawaza “Labda nikimkalia kimya atapata nafasi ya kuwa na mwanamke mwingine!” Hapana, sisemi umkalie kimya lakini uache kumkalia kooni.

Mpigie simu ukimmiss, msalimie na ukimkumbuka umtumie meseji. Lakini achana na mambo ya “Siku hizi umebadilika! Utakua na mwanamke mwingine! Nataka kuja kwako una nafasi! Niko njiani nakuja kwako! Naomba basi kuonana!”

Yaani yale mambo ya kuonyesha kuwa umechanganyikiwa, maisha yamesimama yanamfanya mwanaume sio tu kukuchoka bali kuona “Huyu hata nikimfanyia vituko, hata nikitembea na Dada yake hawezi kuniacha mbona kachanganyikiwa hivi?

LAKINI KUNA WANAUME WANAPENDA HIVI KUFUIATILIWA!

Ni kweli, kuna baadhi ya wanaume wanapenda kufuatiliwa, yaani anaringa ili umpigie simu mara kumi. Fanya kwa kipimo, ubaya ni kuwa, ukifanya sana baada ya muda utachoka. Kwamba k**a kila siku utakua ni mtu wa kumfuatilia, kumpigia simu mara mia utachoka na mahusiano yataisha.

Kwa leo tuishie hapa, naamini umejifunza kitu, “HAKUNA KUACHWA ACHWA”

JINSI KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOATendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii hu...
16/03/2022

JINSI KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Tendo la ndoa ni tendo lenye ladha ya pekee kwa mwanadamu, kufika kilele hali hii huwa haichukui dakika ni kitendo kinachojiri ndani ya sekunde 30 haswa kwa mwanaume na kwa mwanamke huzidi kiasi kuna sababu yake ntaelezea baadae. Sasa tendo hili kwa mwanamke ni k**a kuonyesha maridhio ya nafsi yake kwa ampendae.

Mwanaume humchukia mwanamke kwakuwa hataki tendo la ndoa na mwanamke humlaumu mwanaume kuwa hajui kupenda. Mwanaume humlaumu mwanamke kuwa huongelea tu mapenzi lakini hajui kuyafanya hayo mapenzi anayo yataka. Sababu ya mwanadamu kutaka kufanya tendo la ndoa ni homoni iitwayo "testosterone" ambapo mwanaume huzalisha mara 20 zaidi ya mwanamke anavyozalisha yaani mwanaume akifanya leo akashinda kesho atajiona sawa na mwanamke alie fanya leo na kupumzika siku 20 bila kufanya.

Sasa kimaumbile mwanaume huwa ni mwenye kuhitaji sana tendo hili na mwanamke huitaji baada ya kuona kua anapendwa ndo maana Mungu alisema "Wanaume wapendeni wake zenu". Najua hulka ya kiume ni kufukuzia mwanamke k**a afanyavyo mnyama wa porini utasumbuliwa na utakimbiza labda kwa mda mrefu ila unapo mpata unashangalia na kula kwa furaha ila hamu ile huisha kadiri siku zinavyozidi kwenda (naongelea waliopo kwenye Ndoa )

Na mwanamke nae huwa na manjonjo mengi mwanzoni na akiona sasa nimeshateka mipaka yote ya nchi hii hujisahau na kutulia kitu ambacho humfanya mwanaume kujiuliza vipi mke ameshapata wa pembeni japo sio hivyo. Sasa ili kudumisha ndoa iwe ni yenye kudumu hakikisha mwanaume una mfukuzia mkeo yaani (Yaani unamfanyia vile vitu ulivyokuwa unamfanyia kabla ya kumpata k**a vile unamtoa dina, una mpeleka sehemu nzuri ambayo hajawahi fika na usione haya kumshika au kumchumu mkeo ni wako bhana na hakika yeye hujisikia raha sana na utadumu nae muda mrefu bila kuona usaliti labda iwe tabia yake).

KWA NINI NIMEONGELEA MAMBO HAYA

Tambua kuwa ili uweze kushinda kwenye mchezo wowote unahitaji maandalizi ya kutosha. Mechi ambayo hujaipigia tizi una asilimia kubwa ya kufungwa yaani hata k**a ungekuwa umefundwa yote kuhusu tendo la ndoa na k**a hakuna mapenzi ndani ya nafsi ya mwanamke una asilimia ndogo ya kumfikisha kilele. Kisha baada ya hayo Muumba wetu anasema "amelaaniwa anae muingilia mke wake bila kumuandaa" yaani zipo sehemu zaid 21 za zinazompa raha na hamasa ya kushiriki tendo la ndoa kwa mwanamke usikimbilie tu kwa bibi.

K**a hayo yote yamefanyika na bado basi huenda kukawa na tatizo hivo ni vema kuchukua hatua.

HUDUMA YA KWANZA

Chukua Kungu Manga robo kile na Karanga nusu Kilo.

KISHA CHANGANYA lakini Kungu Manga itabidi UTWANGE na karanga USITWANGE,
kisha tafuna pamoja nusu saa au saa moja kabla ya kushiriki tendo la ndoa utapata raha na hisia za ajabu na kufurahia tendo hilo. Endelea kutumia mchanganyiko huo kwa Muda wa siku 11 basi kwa Uwezo wa Mungu utakuwa umepona kabisa tatizo hilo la kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Address

Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dr. Amar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Practice

Send a message to Dr. Amar:

Share

Share on Facebook Share on Twitter Share on LinkedIn
Share on Pinterest Share on Reddit Share via Email
Share on WhatsApp Share on Instagram Share on Telegram