17/11/2023
*MAJI BARIDI : Je, Wewe Ni Mpenzi Wa Kunywa Maji Baridi...?*
Watu waliopo ukanda wa baridi huburudika sana endapo atakunywa maji ya bariiiiidi na kujiskia fahari sana.
Baadhi ya watu hupendelea kushushia na maji ya bariiiidi mara tu wamalizapo kula. ๐๐
Utaufrahisha ulimi wenye urefu wa Sentimita 7 tu na kuusumbua utumbo wenye urefu wa Mita 7. Twende kwenye mada kuu. ๐๐ผ๐๐ผ
Ukinywa maji ya baridi muda mfupi kabla ya kula au baada ya kula chini ya nusu saa hugandisha mafuta yaliyomo kwenye chakula. Hii hupelekea kuongezeka uzito, choo kigumu sababu ni umeng'enyaji mbovu wa vyakula tumboni.
USHAURI KWAKO: Kunywa Maji Ya Vuguvugu Kupata Faida Hizi...! ๐๐ผ๐๐ผ
1. Huondoa sumu mwilini
Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwezesha viungo k**a vile figo kufanya kazi yake vyema.
2. Huboresha ufyonzwaji chakula
Kufyonza chakula; ni mchakato ambao mwilli hutumia vyakula (wanga, protini na mafuta) ili kupata nguvu na kujijenga. Hivyo basi, unywaji wa maji huwezesha mchakato huu kwenda vyema na kuufanya mwili kuwa na afya njema.
3. Husaidia kupunguza uzito
Soda ina sukari gramu 35 na gramu 140 za kalori ikilinganisha na maji ambayo vyote ni sifuri. Hivyo basi, ni vyema ukapendelea kunywa maji zaidi kuliko vinywaji vingine vya viwandani.
4. Huondoa kiungulia na matatizo ya umengโenyaji wa chakula
Unywaji wa maji utarahisisha na kuhimiza mchakato mzima wa umengโenywaji wa chakula.
5. Huzuia mawe kwenye figo
Ili kurahisisha utendaji kazi wa figo zako pamoja na afya yake, zingatia kunywa maji ya kutosha hasa asubuhi.
6. Huongeza kinga ya mwili
Kujijenga kwa kinga, mwili hutegemea sana maji. Hivyo ni vyema kuhakikisha unaongeza kinga ya wili wako kwa kunywa maji ya kutosha hasa kabla ya kula kitu chochote.