04/02/2023
VIDONDA VYA TUMBO -AINA, CHANZO, DALILI & TIBA
UTANGULIZI – UJUE UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, k**a ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.
Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine k**a kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.
AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO
Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)
Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa

2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;
Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu k**a asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
Kuwa na mawazo mengi
Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
Kunywa pombe na vinywaji vikali
Uvutaji wa sigara
Kuto kula mlo kwa mpangilio
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili k**a;

Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa k**a ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana,
0742886127
Kwa tiba na ushauri.