27/03/2023
DALILI ZA KANSA.
Hizi ni dalili tu na sio lazima ziwe ni ugonjwa wa kansa lakini kikubwa ni kwenda hospitalini kwa vile uwezekano upo.
Hizi ni pamoja na :
1:KIKOHOZI/ MABADILIKO YA SAUTI
Kukohoa muda mrefu na pia hali hii ikaifanya sauti kuwa nzito, nyepesi au kukwaruza na hata kukwama si ya kupuuzwa.
Japo kikohozi wengi hakiwahofishi, kukohoa kwa muda mrefu na kupata makohozi yenye damu ni dhahiri jambo la kuhofiwa.
"Vikohozi vingi si kansa," anasema Therese Bartholomew Bevers, dakati na profesa wa kuzuia saratani katika taasisi ya Underson Cancer Center. "Lakini kwa hakika kukohoa makohozi yenye damu mara kwa mara kunahitaji kuchunguzwa na kuangaliwa k**a kuna saratani ya mapafu inayojitokeza.
Ni lazima bingwa achunguze mapafu kwa xray au kwa CT scan kufahamu hatari ama uwezekano wa saratani unaohofiwa.
2. MATATIZO YA KUPATA CHOO
Iwapo tumbo lako litakuwa na mabadiliko kwenye utaratibu wa kupata haja usizubae tafuta tiba. Inaweza kuwa kuhara mara kwa mara, choo kupungua au kuwa na choo kidogo au kukosa haja kubwa inaweza kuwa ni tatizo kwenye utumbo mpana, anasema Bartholomew Bevers.
"Inawezekana kuna uvimbe unaozuia haja kupita kwenye utumbo na kusafiri ili kutoka nje. Huu ndiyo wakati wa kufanyiwa kipimo kinachoitwa colonoscopy kuona k**a kuna uvimbe tumboni.”
3:MABADILIKO KWENYE HAJA NDOGO
"K**a kuna damu kwenye mkojo inawezekana ni saratani ya kibofu ama ya figo japo katika hali ya kawaida wengi hudhani ni tatizo la maambukizi ya njia ya mkojo UTI” Bartholomew Bevers, anaongeza.
4.MAUMIVU YA MUDA MREFU
"Si maumivu yote ni saratani lakini yale ya muda mrefu na ya mara kwa mara tena eneo moja ni lazima kuyachunguza “,Bartholomew Bevers. Mathalani ukiwa na maumivu ya mara kwa mara kichwani si kwamba una saratani ya kichwa lakini kuna jambo la kuangaliwa.
Aidha, maumivu makala kifuani pengine ni dalili ya saratani ya mapafu, pia maumivu ya mara kwa mara kwenye tumbo chini ya kitovu yaweza kuashiria saratani ya kifuko cha mayai.
5:MABADILIKO YA VIVIMBE
K**a una kivimbe au kipele usoni au popote kwenye ngozi lakini ghafla kinabadilika na kuanza kukua na kubadilika usisite kukitafutia tiba. Ni vyema kumpelekea mtaalamu wa ngozi vivimbe hivyo.